I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Sunday, June 13

TFF YAINGIA HASARA MECHI YA BRAZIL NA TAIFA STARS

HUU NDIO MPANGO MZIMA
Shirikisho la kabummbu nchini TFF leo limekubali kwamba limekula hasara kutokana na kuandaa mechi ya Brazil na Taifa Stars ambapo kiasi cha shilingi 1.6bn/- tu kati ya takriban 4bn/ zilizotarajiwa. Katibu Mkuu wa TFF Frederick Mwakalebela kasema sasa hivi jijini Dar kwamba Shirikisho hilo linajiandaa na mikakati ya kufunika hasara hiyo pamoja na kuweka mambo sawa.
Hakutaka kwenda kwa undani ni shilingi ngapi walikopa na toka wapi lakini kasema Brazil walilipwa pesa yao kwa muda Muafaka na kwamba watoa huduma wote walishalipwa na hakuna mwenye kuidai TFF.
Kasema, hata hivyo, mechi hiyo na Brazil ilikuwa na faida kubwa ya muda mrefu, ikiwa ni pamoja ya wachezaji takriban 6 kufuatwa na mawakala wa timu za ulaya kuwataka. Pia amesema utalii utakuwa sana kwani wengi wanaulizia Tanzania.