I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Monday, June 7

Joe Biden kuzuru Kenya

Makamu wa Rais wa Marekani, Joe Biden

Makamu wa rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuwasili mjini Nairobi hii leo. Biden anawasili kutoka nchini Misri na atamalizia ziara yake ya Afrika nchini Afrika Kusini ambapo atawakilisha taifa lake katika hafla ya ufunguzi wa kombe la dunia.

Akiwa jijini Nairobi, Biden anatarajiwa kutoa taarifa juu ya marekebisho ya katiba na mageuzi mengine. Pia anatarajiwa kukutana na rais wa Sudan ya kusini Salva Kiir na kuhudhuria mkutano muhimu juu ya Somalia.

Duru kutoka Nairobi zinaarifu kuwa katika mkutano wao na Biden, viongozi wa Kenya watasisitiza athari za mzozo wa Somalia katika kanda hii.