Timu ya Taifa ya Brazil imefanya kile ambacho kilitarajiwa na watu wengi au mashabiki wengi wa soka nchini baada ya kuifunga Taifa Stars bao 5-1.Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wachache ambao inawezekana labda kutokana na kingilio ambacho kimewekwa na TFF kuwakwaza mashabiki wengi kutokwenda kuishangilia timu yako kutokana na kipato kuwa kidogo.Taifa Stars ilianza mpira kwa kasi lakini Brazil ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kutoka kwa Robinho,Bao la pili limefungwa tena na Robinho na la tatu limefungwa na Remirez,la nne limefungwa na Ricardo Kaka na bao la kufutia machozi la Stars limefungwa na Jabir Aziz kalamu ya magoli ilihitimishwa na Ramirez kwa kufunga goli la tano.Mpaka mwisho wa mpira Brazil 5 Stars 1
Dakika za mwisho mwisho mpra kumalizika watu wakiwa hawaamini kilichotokea