Msanii wa Filam Tanzania Juma Chikoka ametangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Ilala kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi {CCM}.Juma chikoka ambaye ameshiriki movie nyingi kama vile My Dream,Fake Promise,Danger Zone na nyingine nyingi vilevile ni Producer wa movie nchini.Akitangaza nia hiyo Juma Chikoka ama Chopa ambaye ana elimu ya Digrii ya Sanaa katika chuo kikuu cha Bangalore nchini India amesema kuwa "Maendeleo kusuasua katika kila nyanja ndio yaliyomsukuma kama kijana kujitolea kwa hali na mali kuwatumikia wananchi wa Ilala..naomba support yenu wananchi wa ilala na wasanii wenzangu".Huyo ndiyo Juma chikoka tumuunge mkono jamani katika mbio zake hizo za kuwania ubunge Hapa akiwa masomoni nchini India Akiwa katika shughuli zake za kisanii