Hukumu ya kwenda gerezani na kutumikia kifuncho cha miaka miwili jela ndiyo adhabu anayoanza kuitumikia aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala katika Benki Kuu ya Tanzania BoT Amatus Liyumba, baada ya kupatikana na hatia ya kutumia vibaya madaraka aliyokuwa nayo wakati akiwa kazini, hususana wakati wa ujenzi wa maghorofa pacha ya BOT jijini Dar. Hata hivyo leo hii katika mahakama hiyo, mahakimu watatu wanaounda jopo la mahakimu linalosikiliza kesi hiyo, walitofautiana huku wawaili kati yao wakiwa na mtazamo mmoja wakati wa uandikaji na usomwaji wa hukumu yao. Wawili hao ambao ni hakimu Benedict Mwingwa pamoja na Lameck Mlacha, waliandika na kusoma hukumu iliyofanana ambayo kimsingi ndiyo iliyomtia hatiani Liyumba na kumsababishia kupata adhabu hiyo. Kwa upande wa Hakimu Mkasimongwa ambaya ndiye aliyekuwa kiongozi wa jopo hilo la mahakimu, ndiye aliyeandika hukumu yake tofauti hukumu ambayo ilionesha kumuachia huru mshatakiwa kwa kuwa hana hatia. Lakini kutokana na nafasi kubwa na kuungwa mkono iliyoonekana na mahakimu wawili, ilisababisha mahakama hiyo kuichukua kiutekelezaji hukumu ya mahakimu hao Mlacha na Mwingwa na kumuhukumu Liyumba kifungo hicho. Akisoma hukumu hiyo iliyomtia hatiani Liyumba, Hakimu Mlacha alisema kuwa ushahidi wa mashahidi nane wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo, ndivyo vilivyopelekea mahakama kumtia hatiani mshtakiwa huyo. Mlacha alisema kuwa, alisema kuwa Liyumba alisahini barua za mahidhinisho ya ufanyikaji wa mabadiliko ya ujenzi wa jengo la BoT, wakati hakiwa hana mamlaka ya kufanya hivyo. Aliongeza kuwa barua hizo zilikuwa na sahihi yake Liyumba jambo ambalo ni kinyume kwani ilitakiwa ziidhinishwe na bodi ya benki na si kurugenzi kama ambavyo alikuwa akifanya Liyumba. Pia mahakama hiyo iliukataa ushahidi wa utetezi uliotolewa mahakamani hapo na Liyumba, ushahidi ambao ulidai kuwa mammlaka ya kusahini barua hizo, alipewa na aliyekuwa Gavana wa benki hiyo Daud Balali kwa njia ya mdomo. Mlacha alisema kuwa mahakama imeingia mashaka juu ya kuamini hilo, kutokana na ukweli kuwa BoT ni taasisi ambayo kulingana na ukubwa wake na uzito wake hisingeweza kutoa maamuzi au kuumpa mtu madaraka makubwa pasipo kutumia maandishi hili kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa Mahakama hiyo inauchukulia ushahidi wa utetezi uliotoewa mahakamani hapo, si wa kweli kwani hata mmoja wa mashahidi wa upande wa mashtaka aliithibitishia mahakama hiyo kuwa maelekezo ya Gavana yalikuwa yakitoka kwa barua. "Hata shahidi wa nne wa upande wa mashtaka bwana Michale Shirima, ambaye alikuwa mjumbe wa bodi ya benki, aliithibitishia mahakama hii kuwa maamuzi ya Gavana yalikuwa yakitolewa kwa maandishi na si kwa mdomo kama Liyumba alivyotuambia"alisema Mlacha. Mbali na hilo, mahakama pia iliukataa ushahidi wa shahidi wa pili wa utetezi ambaye ni aliyekuwa Katibu wa Benki bwana Bosco Kimela, kwa kuita ushahidi huo kuwa ulikuwa wa kutungwa na mstakiwa pamoja na shahidi huyo. Mlacha alisema kifungu namba 96 (1) cha Kanuni ya adhabu, kinasema kwamba iwapo mtu aliyeajiriwa katika taasisi ya umma, akielekeza kufanyika kwa jambo kinyume na sheria na taratibu za ofisi na hivyo kusababisha madhara kwa mtu mwingine, atakuwa ametenda kosa. Aliongeza kuwa baada ya kupitia kwa makini kifungu hicho, mahakama imeona kuwa kosa alilotenda Liyumba lilikuwa ni kinyume na sheria na kwamba lilileta madhara kwakuwa gharama za ujenzi wa jengo hilo zilipanda kulinganishwa na zile zilizopangwa kwenye mkataba uliopitishwa na bodi hapo awali. Kwa upande wa Wakili wa utetezi Majura Magafu, kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo aliiomba mahakama hiyo kupanga adhabu kwa kuangalia kifungu cha 38 (1) 16 ambacho kinairuhusu mahakam kutoa adhabu ya faini, ama kifungo cha nje kwa mashtakiwa. “Muheshimiwa tunaiomba mahakama iweza kukiangalia kifungu hicho na kumpa mshatakiwa adhabu ya kulipa faini, au kifungo cha nje hasa ikizingatiwa umri wa mshtakiwa ni wa miaka 62 na vilevile anamaatatizo ya kiafya. Magafua alidai kuwa mahakama izingatie kwamba Liyumba nategemewa na familia yake. Lakini mambo yalikuwa tofauti wakati wa upangaji wa adhabu hiyo, ambapo Hakimu Mlacha na Mwingwa walipingana na maombi hayo ya magafu. Pamoja na maombi hayo kwa mahakama, Hakimu Mlacha alitoa adhabu ya kifungo hicho baada ya kusema kuwa mshtakiwa hasingeweza kulipa faini hasa ikizingatiwa kuwa hivi sasa kuna mapambano ya vitendo vya rushwa. Kwa upande wa Hakimu Edson Mkasimongwa, alisoma huku yake aliyoiandaa ambayo ilipingana na hukumu ya awali, ambapo pia ilisomwa hili kutunza kumbukumbu za mahakama. Mkasimongwa alisema kuwa upande wa mashataka umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi ya Liyumba, hivyo anatakiwa awe huru kutokana na hilo. Mkasimongwa alipingana na hoja ya kuwa mshtakiwa alisahini barua za kuhidhinisha kufanyika kwa mabadiliko wakati akiwa hana mamlaka hayo, kwasababu haikuwa na msingi. Aliongeza kuwa kwa upande wa hilo, yeye haoni kama ni kutenda kosa la matumizi mabaya ya ofisi kwani Liyumba kama mkuu wa kurugenzi iliyokuwa ikisimamia ujenzi huo alikuwa na na mamlaka ya kusahini barua hizo kama aliona kuwa hazikuwa na ubishani. Hukumu hizo zilipomalizika kusomwa , Liyumba aliondoka mahakamani hapo huku akilindwa na askari kuelekea kwenye gari la magereza.