I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Friday, May 14

Sean kingstone kuanza makamuzi vilivyo jmosi diamond jubilee

Sean Kingstone akiwa ameambatana na bodi gadi wake pichani kulia,wakirejea hotelini mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandishi wa habari mapema leo asubuhi
Eeeh bwana hapa vipi,mie nikiwa nimepigwa konozzz na mkali wa swagazzz Sean Kingstone leo
Mwanamuziki Sean Kingston katikati akiwa na Mkurugenzi wa Masoko wa TBL David Minja kushoto na Meneja wa kinywaji cha Kiliamanjaro Premium Lager George Kavishe baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari ,Mwanamuziki huyo yuko nchini kwa mwaliko wa TBL kwa ajili ya kushiriki katika utoaji wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards zitakazofanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Sean KingStone akiteta jambo na Meneja wa kinywaji cha Kiliamanjaro Premium Lager George Kavishe,kabla ya mkutano na waandishi wa habari kuanza mapema leo asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree,Oysterbay jijini Dar
Mwanamuziki kutoka nchini Marekani Sean Kingstone na Wenyeji waliomleta hapa Nchini Kampuni ya Bia ya TBL,wakizungumza na waandishi wa habari mapema leo asubuhi ndani ya hoteli ya Double Tree,Oysterbay jijini Dar kuhusiana na onesho la mwanamuziki huyo wa kimataifa,Sean Kingston atakuwepo kesho kwenye utoaji tunzo kwa wasanii watakaoibuka kidedea na jumamosi atakamua ndani ya ukumbi wa diamond jubilee jijini Dar.