Staa ‘hot and sexy’ wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe (pichani), amebambwa laivu akicheza bao kwenye mchanga na mtoto aliyejulikana kwa jina moja la Zainabu ambapo alipigwa bao 2-1. Tukio la Wolper kunaswa na kamera yetu akicheza mchezo huo unaopendwa zaidi na wazee lilijiri maeneo ya Hananasif-Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo staa huyo alikwenda kumtembelea msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anayeishi pande hizo. Akiwa anamsubiri ‘shosti’ wake aliyekuwa akijikwatua, tayari kwa mtoko wa jioni, Wolper mwenye zaidi ya filamu 30 alizocheza, aliamua kumchomoka ndani na ‘stuli’ kisha kuungana na watoto waliokuwa nje wakijiburudisha na mchezo huo kwa lengo la kuwaonesha ujuzi wake. Hata hivyo, hadi mwisho wa mchezo, Wolper aliambulia kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Zainabu katika michezo mitatu ya mpambano wao. Papzrazi wetu alipomtokea Wolper ili kujua kulikoni kugaragazwa na mtoto huyo tena mchangani bila kujali bakteria na vumbi, staa huyo alikuwa na haya ya kusema: “Ki ukweli naupenda sana mchezo huu, ndiyo kitu pekee ambacho huwa nakifanya nikiwa nimepumzika nyumbani kwangu au ninapokuwa sina ratiba ya ‘location’ (sehemu ya kuigizia). “Haya ndiyo mazingira ya nchi yetu, mimi sina mapozi na kama ningejidai kutumia ‘glovusi’, ingekuwa ni kumbagua ninayecheza naye.”