I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Wednesday, December 29

Baada ya yote vijisenti abusu mahakama kwa laki 7

Mbunge wa Bariadi Mashariki na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Mhe. Andrew Chenge, leo asubuhi ametiwa hatiani na Hakimu wa Mahakama ya Kinondoni kwa makosa manne ya barabarabi, yakiwemo ya mauaji ya wasichana wawili aliowagonga kwa gari alilokuwa akiendesha na kuwaua, Machi 27, 2009, jijini Dar es salaam. Chenge ametiwa hatiani kwa makosa manne ya Kusababisha vifo vya wasichana wawili, Kugonga Bajaji, Kuendesha gari kwa uzembe na kuendesha gari isiyokuwa na Bima. Makosa yote hayo amepigwa faini ya shilingi za Kitanzania laki saba! (700,000/=) na amelipa.


gari la Chenge lilohusika katika ajali hiyo


Bajaji iliyogongwa na kuua abiria wawili waliokuwemo, ambapo dereva alipona na hakupatikana hadi leo.