I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Thursday, December 30

kumbe ganda la katiba ya tz liko hivi...!!!..unajua ukurasa wa kwanza kabla haijafanyiwa mabadiliko???


Ni matumaini yangu watanzania wenzangu mu-wazima wa afya. Leo najitokeza tena, najitokeza nikiwa na maneno machache ya kuwaambia wananchi wenzangu.

Kwanza kabisa nitakuwa mchache wa shukurani kama nitaacha kuwashukuru wale wote wanaovutiwa na kufurahia makala zangu mbalimbali. Mungu awabariki na kuwapa afya njema.

Ni wiki kadhaa sasa tangu vuguvugu la wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani kuzidisha mbiu ya madai ya katiba mpya.

Lakini kwa maoni yangu hapa naona kuna walakini kidogo, tunafahamu kuwa katiba ni haki ya watanzania wote.

Lakini mamilioni ya watanzania hawajawahi kuona hata paragrafu moja ya katiba hiyo achilia mbali ukurasa mzima.

Nadhani ingelikuwa ni bora zaidi kuanza kudai machapisho ya katiba yenyewe ili kila mwananchi apate fursa ya kuisoma na kubani mapungufu yake ili kila mtu apate
nafasi ya kutoa maoni yake

Leo hii katiba imefanywa kuwa siri kubwa, siri ambayo hata wenye katiba wenyewe wananchi hawatakiwi kuiona.

Kufichwa kwa katiba hiyo ni kielelezo cha mapungufu yake.

Iwekwe wazi, wananchi waisome ili watoe michango yao na hatimaye mchakato wa mabadiliko uanze rasmi.

Ama yote mawili yafanyike kwa pamoja, kudai katiba iwekwe wazi na kudai mabadiliko yake kwa pamoja. Vinginevyo tutakuwa tunadai mabadiliko ya kitu tusichokijua.