I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Thursday, December 30

kumbe ganda la katiba ya tz liko hivi...!!!..unajua ukurasa wa kwanza kabla haijafanyiwa mabadiliko???


Ni matumaini yangu watanzania wenzangu mu-wazima wa afya. Leo najitokeza tena, najitokeza nikiwa na maneno machache ya kuwaambia wananchi wenzangu.

Kwanza kabisa nitakuwa mchache wa shukurani kama nitaacha kuwashukuru wale wote wanaovutiwa na kufurahia makala zangu mbalimbali. Mungu awabariki na kuwapa afya njema.

Ni wiki kadhaa sasa tangu vuguvugu la wanasiasa hasa wa vyama vya upinzani kuzidisha mbiu ya madai ya katiba mpya.

Lakini kwa maoni yangu hapa naona kuna walakini kidogo, tunafahamu kuwa katiba ni haki ya watanzania wote.

Lakini mamilioni ya watanzania hawajawahi kuona hata paragrafu moja ya katiba hiyo achilia mbali ukurasa mzima.

Nadhani ingelikuwa ni bora zaidi kuanza kudai machapisho ya katiba yenyewe ili kila mwananchi apate fursa ya kuisoma na kubani mapungufu yake ili kila mtu apate
nafasi ya kutoa maoni yake

Leo hii katiba imefanywa kuwa siri kubwa, siri ambayo hata wenye katiba wenyewe wananchi hawatakiwi kuiona.

Kufichwa kwa katiba hiyo ni kielelezo cha mapungufu yake.

Iwekwe wazi, wananchi waisome ili watoe michango yao na hatimaye mchakato wa mabadiliko uanze rasmi.

Ama yote mawili yafanyike kwa pamoja, kudai katiba iwekwe wazi na kudai mabadiliko yake kwa pamoja. Vinginevyo tutakuwa tunadai mabadiliko ya kitu tusichokijua.


Show it ...at new year 2011!!!!!!

HapPy B.dAy ....Bakari Changale

Mr Bakari Changale
Leo ni siku ya kuzaliwa BAKARI CHANGALE 30.12....Blog hii na kwa niaba ya ma class mate wake wote waliosoma nae Mkwakwani sec sch Tunamtakia furaha yeye na familia yake yte,Mmungu ampe afya njema ktk maisha yke na mafanikio ktk siku zake nyingine za usoni.


We wish u happy b.day BECKA

Wednesday, December 29

Baada ya yote vijisenti abusu mahakama kwa laki 7

Mbunge wa Bariadi Mashariki na aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria, Mhe. Andrew Chenge, leo asubuhi ametiwa hatiani na Hakimu wa Mahakama ya Kinondoni kwa makosa manne ya barabarabi, yakiwemo ya mauaji ya wasichana wawili aliowagonga kwa gari alilokuwa akiendesha na kuwaua, Machi 27, 2009, jijini Dar es salaam. Chenge ametiwa hatiani kwa makosa manne ya Kusababisha vifo vya wasichana wawili, Kugonga Bajaji, Kuendesha gari kwa uzembe na kuendesha gari isiyokuwa na Bima. Makosa yote hayo amepigwa faini ya shilingi za Kitanzania laki saba! (700,000/=) na amelipa.


gari la Chenge lilohusika katika ajali hiyo


Bajaji iliyogongwa na kuua abiria wawili waliokuwemo, ambapo dereva alipona na hakupatikana hadi leo.





Thursday, December 23

May this season bring u success ,gud tym & happiness...Marry xmass & happy new year.





Soma chachandu ,vikuku na vichele vya Xmass na New year


Ni kweli kabisa kwamba, kwa wapenzi walioshibana kila siku ni sikukuu kwao. Hata hivyo, sina budi kuwakumbushia baadhi ya mambo ambayo ni vyema wakafanyiana katika siku hizi za sikukuu nikiamini kwamba, wakiyafanya watakuwa katika nafasi nzuri ya kulifanya penzi lao lionekane jipya. Tokeni muende kokote Yawezekana katika kipindi chote cha uhusiano wenu hamjawahi hata siku moja kutoka pamoja kwenda kwenye ukumbi wa starehe ama sehemu yoyote tulivu. Kimsingi kutoka na mwenza wako kuna faida kubwa sana, hivyo basi si vibaya katika sikukuu hizi zinazokuja mkajiandaa kwa kutenga fedha ambazo zitawafanya siku hiyo muende sehemu ambayo hamjawahi kwenda pamoja. Kama wewe na mwenza wako mlikuwa na utaratibu wa kwenda ‘out’ kila wikiendi, safari hii mnaweza kupanga kwenda sehemu tofauti, ikiwezekana hata kutoka nje ya mji mnaoishi. Kuna mengi ya kufanya mnapotoka ‘out’, mojawapo ni kubadilishana mawazo juu ya maisha yenu, kuombana msamaha pale ambapo mlitokea kutofautiana. Yaani ni kipindi cha kulikarabati penzi lenu na hata pale mtakapokuwa mnarudi itakuwa ni kama vile mmefungua ukurasa mpya. Kununuliana zawadi Siku zote zawadi ni chachandu katika penzi. Kumbuka kwamba katika suala la uhusiano, zawadi ni zawadi bila kujali ukubwa wake. Hii itategemea tu na uwezo wako. Kwa maana hiyo basi ni vizuri ukamwandalia zawadi nzuri mwenza wako ambayo itamfanya afunge na kufungua mwaka mpya kwa matumaini kwamba kweli unampenda. Kadi za Sikukuu Hili kwa wengine ni kama kuwakumbushia. Unapaswa kumwandalia mpenzi wako kadi ya kumtakia Krismasi njema na mwaka mpya wenye furaha. Kumbuka kadi utakayomnunulia mwenza wako inatakiwa kuwa tofauti na ile utakayompelekea rafiki yako wa kawaida au mzazi wako. Ni muhimu sana kulizingatia hili. Angalia rangi za kadi, ujumbe na ukubwa wa kadi. Hakikisha kadi utakayompelekea laazizi wako inamvutia na kumfanya atamani kuisoma kila mara kutokana na jinsi ilivyo. Mfanyie ‘surprise’ Rafiki yangu mmoja amenieleza kwamba, katika Sikukuu ya Mwaka mpya anatarajia kumshangaza mpenzi wake ‘surprise’ kwa kumtamkia kwamba, wakati umefika wa wao kufunga ndoa. Wewe umejiandaa kumfanyia ‘surprise’ gani mpenzi wako? Ni siku za furaha Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, hakuna kitu kibaya kama wapenzi katika siku hizi kununiana ama kuudhiana. Hizi ni siku za furaha hivyo basi, hakikisha unafanya kila uwezalo kumfanya mwenza wako awe na uso wa tabasamu muda wote. Hivi itakuwaje pale mtakapokuwa mnaposherehekea Sikukuu ya Mwaka mpya kisha mpenzi wako akababatiza ujumbe wa mapenzi katika simu yako kutoka kwa mtu mwingine? Ikitokea hivyo itakuwa ni nuksi kwa mwaka mzima. Ndio maana nasema jitahidi sana katika sikukuu hizo kuyaondoa yale makovu yaliyokuwa katika penzi lenu ili muingie katika mwaka mpya penzi lenu likiwa na uhai mpya. Hakikisha tu unajiandaa vizuri na ndiyo maana nimeamua kuandika makala haya mapema kabisa. Labda kwa kumalizia niseme tu kwamba, kila atakachokufanyia mwenza wako, kiwe kidogo ama kikubwa ni vyema ukakithamini. Ni hayo tu, nawatakia Krismasi njema na mwaka mpya wenye mafanikio.

Wednesday, December 22

Unajua kwenye ma***nzi kuna asali, limao na shubiri?


Umeoa au umeolewa? Unataka kuolewa au kuoa? Ndiyo maswali ambayo leo ninakuuliza wewe unayeperuzi ukurasa huu. Lengo langu ni kuongea na wale wote walioamua kufunga ndoa na wale wengine ambao wako mbioni kufanya hivyo. Namaanisha waliofunga ndoa na wanaotaka kufunga ndoa, tukianza na wale ambao hawajafunga ndoa nawakata wajue kwamba ndoa si kitu cha kukifanyia majaribio kwa kukichezea kama vile ambavyo wanandoa wengi wa siku hizi wanavyofanya. Nafahamu kwamba kuna vijana na wasichana wengi ambao wanatamani kuingia kwenye ndoa huku wakiwa na imani kwamba wakifunga ndoa wataishi maisha ya raha mustarehe kama wanavyowaona wengine wanavyoishi, wenyewe wana msemo wao unaosema ‘wakubwa wanafaidi’. Kwako wewe binafsi kabla ya kuingia kwenye ndoa, unatakiwa kuwa makini na mtu ambaye unamchagua kutaka kuwa ubavu wako wa pili, unamfahamu vipi uelewa wake katika na suala zima la mapenzi. Unafahamu kwamba anayekuoa anaweza kuachana na wewe pamoja na kwamba hivi sasa mnapendana kiasi cha kufikia kuwaona watu wengine hawapendani zaidi yenu? Je, wewe na yeye mnajua kama mapenzi yamegawanyika katika ‘stage’ mbili zisizo rasmi za furaha na maumivu? Ambazo matawi yake ni asali, limao na shubiri? Ndiyo penzi linapoanza linakuwa tamu kama asali, katikati ya mapenzi chachu kama limao na mwisho na mwisho wa mapenzi huwa ni uchungu kama shubiri, je mnayajua haya? Kama mnayajua mnakabiliana nayo vipi, siku zote mimi huwa naamini kwamba penzi ni la Mwenyezi Mungu na kinyume cha penzi ni uadui ambao huletwa na shetani. Je, mnaweza kukabialiana na nguvu za shetani huyo ili ndoa mnayoota kufunga isivunjike? Kuna watu wanaichukulia ndoa kama kitu cha masihara na wala si kitu cha maana ambacho kinaweza kuwafanya kuweza kuendesha maisha yao kwa kufuata kanuni na misingi ya ndoa kama sheria zinavyosema. Nimeamua kusema hivi kwakuwa wanandoa wengi wa siku hizi hawazijui thamani ya ndoa zao walizoziingia, wengi wanachukulia kwamba unaweza kuoa au kuolewa leo na kesho ukaachana bila ya kuona haya wala kuhisi shaka. Kuna hili ambalo linahitaji uangalizi wa kina kabla ya kuingia kwenye ndoa, kwani wapo wanandoa wanaotafuta tiketi ya ndoa kwasababu zao maalumu, kama vile kufuata maslahi fulani au kuondoa mikosi kwa kuwa tu kuna mtu amejiotokeza kwa ajili ya kufunga nao ndoa. Kama hujaingia kwenye ndoa ni heri ukajiuliza mara mbili kwanini uingie kwenye ndoa? Kwanini umuoe au uolewe na huyo unayetaka ufunge naye ndoa? Hapa tunarudi kule kwenye makala yetu ya Jumatano ileee ambayo ilikuwa ikisema kwamba unamependa, anakupenda, mnapendana? Nafahamu kwamba ni vigumu kuingia kwenye ndoa kama mnaotaka kufanya hivyo hamna mapenzi ya kweli, humpendi, hakupendi na wala hampendani. Nilisema kwamba kupenda kunahitaji kujitoa kwako kwa asilimia mia kwa mia kwa mwenzako lakini kujua kama unapendwa kunahitaji ufahamu wa hali ya juu uliojaa ukamilifu wa kuweza kujiridhsisha na kukufanya uthubutu kujiingiza kwenye penzi zito. Pamoja na kwamba hakuna watu wanaopendana moja kwa moja bila ya kukwaruzana lakini mnapofikia katika hatua hiyo huwa mnakuwaje, mnayamalizaje? Hilo ndilo la msingi kabla ya kuvuka hatua kadhaa na kufikia hitimisho la kufunga ndoa. Wanawake wengi wamekuwa wakichezewa na wanaume kwa kuolewa usiku na kuachwa asubuhi na wanaume wengine wamejiamini kwamba wameoa kumbe wanajikuta wao ndiyo wameolewa na wale wanaodai kuwa wamewaoa! Unaweza kushangazwa na hili, lakini ndivyo hali halisi ilivyo katika jamii yetu kwa sasa, mwanaume unaweza kusema kwamba umeoa kumbe umeolewa, mwanamke anakuja kwako kwa lengo la kusaka mali na kisha anakuacha hoi bin taabani kwa kukufilisi kila kitu! Wangapi wamedaiwa talaka na wake zao mbele ya kadamnasi ya watu huku mke akitoa sababu zisizo na msingi na fikra zake zikiwa ni jinsi ya kugawana mali waliyoichuma, umemuoa mwanamke ambaye wala hukumjua vyema familia yake na yeye mwenyewe, mnaburuzana na kufikishana kwa Padri au Sheikh na kutaka kufunga ndoa. Huu ni uhayawani!!! Pamoja na kwamba waswahili wanasema, ukimchunguza kuku humli, lakini kabla ya kumuoa mwanamke kama huyu ulifanya utafiti wa kutosha kwamba anakupenda kweli na ulizijua tabia zake tangu awali? Mwanamke ‘kikwekwelekwe’ anaweza kukusoma udhaifu wako na kisha akakuingiza ‘kingi’ kwa kujifanya anakupenda sana kumbe anapanga kukufilisi kila kitu na kukuacha kapuku kama ‘zizi’ la kufugia kuku, upo? Siyo wanawake tu hata wanaume ‘migumegume’ iliyoshindwa na mitume nao wapo, anakuingia kwa mahaba mazito kumbe kuna kitu kwako amelenga, kwa kuwa wanawake wengi wanapenda kuolewa, basi wakijua kuwa una mali ya kutosha mwanaume anajitosa, siku mbili tatu anakutangazia ndoa. Kwa kuwa wengi wetu tunaendekeza mfumo dume, unakubali kufunga ndoa na mwanaume huyo ‘suruali’ kisha unamuandikisha mali zako, kwa kuamini kwamba mwanaume ndiye uti wa mgongo wa nyumba, basi baada ya muda yuleeee, anakutimua na anatanua na wanawake wengine kwa kutumia mali zako! Hao ndiyo wanaume na wanawake, lazima muwe makini nao katika kuingia katika ndoa zao, kwani ndoa si madoa yatakayoishia kwenye nguo, bali hufika mbali na kuangamiza raho, utakuja kuoneshwa mapenzi mazito kisha ukaachwa huna mbele wala nyuma. Naamini utakuwa na maswali kedekede, utamjuaje mlaghai, utajihami vipi? N.k ni maswali ambayo kwa hakika ni muhimu sana kwako kujiuliza, majibu yake utayapata hapa wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ya mada hii. Utaipenda.

Sunday, December 19

way to ur home.....

Thursday, December 16

WOLPER apigwa bao mchangani


Staa ‘hot and sexy’ wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe (pichani), amebambwa laivu akicheza bao kwenye mchanga na mtoto aliyejulikana kwa jina moja la Zainabu ambapo alipigwa bao 2-1. Tukio la Wolper kunaswa na kamera yetu akicheza mchezo huo unaopendwa zaidi na wazee lilijiri maeneo ya Hananasif-Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo staa huyo alikwenda kumtembelea msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ anayeishi pande hizo. Akiwa anamsubiri ‘shosti’ wake aliyekuwa akijikwatua, tayari kwa mtoko wa jioni, Wolper mwenye zaidi ya filamu 30 alizocheza, aliamua kumchomoka ndani na ‘stuli’ kisha kuungana na watoto waliokuwa nje wakijiburudisha na mchezo huo kwa lengo la kuwaonesha ujuzi wake. Hata hivyo, hadi mwisho wa mchezo, Wolper aliambulia kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa Zainabu katika michezo mitatu ya mpambano wao. Papzrazi wetu alipomtokea Wolper ili kujua kulikoni kugaragazwa na mtoto huyo tena mchangani bila kujali bakteria na vumbi, staa huyo alikuwa na haya ya kusema: “Ki ukweli naupenda sana mchezo huu, ndiyo kitu pekee ambacho huwa nakifanya nikiwa nimepumzika nyumbani kwangu au ninapokuwa sina ratiba ya ‘location’ (sehemu ya kuigizia). “Haya ndiyo mazingira ya nchi yetu, mimi sina mapozi na kama ningejidai kutumia ‘glovusi’, ingekuwa ni kumbagua ninayecheza naye.”

Monday, December 13

REMMY ONGALA AFARIKI DUNIA

Dk. Remmy Ongala enzi za uhai wake.

Mwanamuziki mkongwe nchini,Dk. Remmy Ongala amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo.

Habari za awali zilizofikia mtandao huu zinasema Dk. Remmy alikata roho akiwa nyumbani kwake usiku saa nane na robo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari. Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mipango ya mazishi bado haijajulikana.

Sunday, December 12

Saturday, December 11

Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu kwenye sayari ya vionjo vya kimahaba

Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu endapo wahusika watakuwa wamekubaliana kwa moyo mmoja. Yaani hisia zao ndizo zilizowashawishi kuingia kwenye ‘bwawa spesho’. Kinyume chake ni mateso na ndiyo chimbuko la tuhuma za wanandoa kubakana. Utafiti unaeleza kuwa wanaume wengi huwa hawakubali neno ‘nimechoka’ ambalo ni kawaida kutamkwa na wanawake. Ni lugha ambayo hutumiwa ili kukwepa ushawishi wa wenzi wao ambao huwataka kuingia nao kwenye sayari ya vionjo vya kimahaba. Hata hivyo, lipo jibu la kitafiti kwamba asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa ambao walijaribu kueleza hisia zao kwa ‘mamista’ wao kuwa hawapo tayari kwa tendo, walibakwa. Wakati mwingine hili hubebwa kwa tafsiri kuwa ni jambo la kawaida. Inawezekana hili likawa halipati kujadiliwa sana kwa sababu mpaka leo kuna wanawake bado wanaamini kubakwa na waume zao ni sawa. Kinachowapa unyonge huo ni imani kwamba mwanaume ana haki zote za kimsingi za kuutawala mwili wake. Ziangalieni nyumba nje ya kuta, ndani kuna mengi! “Mwanamke akiolewa haruhusiwi kulala akiwa amevaa kabati!” Ni msemo ambao unavuma mno. Kinachotajwa hapo ni kuwa anayekubali kuolewa, moja ya masharti ni kukubali ombi la mwenzi wake wakati wowote. Ni kweli? Usiku amelala, ghafla anashtuka uzito umeongezeka kifuani, kuangalia, kumbe ni mume anatimiza haja zake! Hiyo ni sahihi? La hasha! Mapenzi hayapo hivyo! Nimesema kuwa tendo la mapenzi linahitaji uhuru wa hisia. Kulazimisha ni kumuumiza. Kukwea juu ya mwenzako bila taarifa ni unyanyasaji. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu mwili wa mwenzake na azitangatie ‘u-tayari’. Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Ila ni vema pia watu wakaelewa kuwa ni kosa kubwa kubania unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo! UTAPOTEZA MVUTO WAKO Tendo ni chachandu! Kwa wanandoa au wapenzi ambao wanaliheshimu hili na kulitekeleza kwa kiwango bora, huwafanya wenzi wao wawe na hisia za karibu kila wanapowafikiria. Hii ina maana ya kuongeza mvuto! Mtu ambaye anakuwa mvivu kutekeleza, mwisho wa siku hupoteza mvuto wake. Kwa asili kila binadamu huwa hapendi usumbufu. Alihitaji penzi la amani, ndiyo maana akawa na wewe, lakini kwa kitendo chako cha kutotaka ‘kachumbari ilike’, maana yake unampa mateso aliyoyakimbia. Anakuomba leo, unamjibu umechoka, kesho tena unaweka ngumu! Hasara kwako hapo ni kupoteza mvuto wa kimapenzi, kwa maana atakapohisi kuhitaji tendo, kila akikufikiria wewe ataona ni mtata na hueleweki, kwamba akikuomba utamtolea nje. Kwa mwanamke ni hatari zaidi, kwani kwa wanaume wasio na uvumilivu, mwisho wa siku huishia kubaka. Hata hivyo, mara nyingi hiyo haiishii hapo, tatizo hukua zaidi na zaidi kulingana na jinsi mgogoro wa kuwekeana ‘kauzibe’ unavyoshamiri ndani ya nyumba. Ukiweza kumudu kumfurahisha mwenzi wako, anachokihitaji umpe kwa wakati. Maana yake atazidi kukuona lulu. Kila akiwa na wewe atajiona yupo huru kuomba huduma wakati wowote. Na pale utakaposema umechoka, itakuwa rahisi kukuelewa na kukuvumilia, kwani siyo kawaida yako. KUSALITIWA NI NJE NJE Unambania kila siku, aendelee kukusubiri kwa kitu gani hasa? Kama ni mwanaume, maua yapo mengi ‘kitaani’, kwahiyo ataangalia kwingine kwa lengo la kutuliza mizuka yake. Ni vema ukitambua kwamba huyo siyo amoeba! Ni mtu hai anayehitaji huduma. Kisaikolojia, ni mwanaume mmoja kwa mia, anayeweza kuvumilia kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi. Asili ya maumbile yao, hasa walio na afya timamu, hisia zao zipo karibu, kwa maana hiyo anaweza kuhitaji hata kila siku. Kama ni mwanamke, ni busara kulitambua hili. Mwanamke anaweza kukaa muda mrefu bila kutamani tendo, lakini hatari kubwa ni kwamba uwezo wake wa kuvumilia ni mdogo mno pale anapokuwa jirani na mwanaume. Akiwa peke yake ni sawa, ila akiwekwa jirani na watu wa jinsia ya pili, mambo huenda kinyume chake. Unafika nyumbani unalala mzungu wa nne, lakini kuna wakati ukigeuka na kumgusa, unamfanya ahisi kutaka huduma. Wewe unambania, hapo utamsababishia akiamka, afikirie mahali ambapo anaweza kupata tiba! Kwa muuza bucha, genge au hata houseboy! Akiitwa barabarani atakuwa mwepesi kusikiliza kwa sababu mwili wake ni mzito na unahitaji kupunguzwa. Akiulizwa kama ana mume, atajibu hana na akisema anaye ataeleza kwamba hana noma! Akiombwa namba atatoa, mwisho wa siku, haki yako atapewa mwingine. Usifikirie maumivu ya kusalitiwa, tafakari kuhusu jinsi unavyodhalilishwa. Kama binadamu na uhusiano wa kimapenzi, heshimu ya kweli ni pale ambapo mwenzi wako anakutunzia ‘tamu’ yako kwenye mazingira yoyote yale. Akiitoa, ni sawa na kuvuliwa nguo! Pale unapopumzika na wengine hutulia hapo hapo! Hii inamaana kuwa hutakiwi kujiuguza uvivu katika suala la mapenzi. Toa huduma inayotakiwa, ikibidi ongeza vionjo kadiri unavyoweza. Kosa kubwa kwa wengi ni kwamba hawachukulii tendo kama ni jukumu la kutekeleza. Yaani ni wajibu! Wanaona ni kitu rahisi ndiyo maana kila siku wanalia.

NEW SONG BONTA.....

Adriana Lima Models $2 Million Dollar Bra

Models $2 Million Dollar Bra. This morning when I turned on the TV I saw the Ariana Lima, the genetically-perfect Victoria Secret Angel, being interviewed while sporting a $2 million bra. Then I noticed that she happened to be in the same Victoria Secret flagship store in Soho that’s just a hop, skip, and jump from the BroBible office. I immediately got on the train and made a bee-line for the store. When I got there you could barely see the Brazilian model thanks to throngs of paparazzi. Determined to snap some photos, I wiggled my way through and I managed to get a few shots of the publicity stunt.

Unfortunately, I wasn’t on the list and they wouldn’t let me into the store to continue collecting photos. If they only knew how much BroBible loves Adriana Lima and all of Victoria Secret’s models they may have been more inclined to let us.

Namitha Kapoor is happy being single

Namitha kapoor
Movie actresses are often linked with their co-stars, which will become a kind of publicity gimmick to the films they act and to their careers as well. But Namitha is one such lady, who was never seriously linked with any star from south India.

Namitha Kapoor was seen in live- in relationship with a photographer named Steffen and then the couple headed for a split due to some reasons, best known to them. Actress Namitha Kapoor, from then on was never linked in any kind of love link up.

For this, the actress feels happy that she is not linked with any actor and also claims that she is not interested in the system of marriage.


Wednesday, December 8

Siku tuliyopewa uhuru wetu Tanganyika 09.12.1961 ilikuwa mwisho wa mwaka


Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na bango
la 'Uhuru Kamili' Tisa Desemba, 1961
Meja Alexander Gwebe Nyirenda akifikisha mwenge wa Uhuru kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro usiku wa kuamkia siku ya Uhuru ili umulike nje ya mipaka yote, uleteeeee tumaini. Meja Alexander Gwebe Nyirenda na mwenye
wa Uhuru alioupandisha Kilimanjaro.
Afande huyu ni mmoja wa mashujaa wa
Uhuru wasioimbwa (Unsung Heroes)

Mwalimu Julius Nyerere na Meja Nyirenda
wakati wa mnuso wa siku ya Uhuru.



BAADA YA UHURU WETU TUKAENDA UGANDA KUMNG'OA HUYU JAMAA..HEBU ONA ANAVYONYONYA MAISHA!!!

Monday, December 6

SIFA NYINGINE ZA KIJINGA.COM

Mara nyingi mazungumzo ya wanaume ni kujisifu kwa Ngono na Ulevi. Unaweza kaa kijiweni na washikaji utasikia oooh mimi nimelala karibu na wanawake wote wa ofisini kwetu na hata mtaani nimechapa sana (anasema haya huku akijua ni uwongo kabisa). Ama mwingine atadakia nimelala jana tu na Khadija na sasa nina miadi na Roselyn (ukifatilia ni uwongo). Hili ni kundi la watu wenye kipato kidogo yaaani wa uswazi.


Ukienda kwa wale wasomi nao ni hivyo nilienda seminar na Ms Rebecca Kule Johannesburg, kwa kweli tulikuwa chumba kimoja ili kusave ila tumerudi hapa bongo tunakaushiana. Mwingine naye atakupa issue Mke wa Fidel ni mtamu sana lile ta.ko acha tu nilikuwa naye Ngurdoto kwenye seminar elekezi si pole pole huu ni uwongo pia. Msomi Mwingine utasikia nina Mademu wawili nimewapata JF week end hii nauwa mmojawapo lol

Pombe

Wengine utasikia mimi kwa pombe ni balaa jana nimekunywa crate la konyagi na konyagi za kopo. Mwingine atachangia acha hizo mimi jana nimepata za kutosha hadi nikafunga bar. Huyu hawa jamaa ukienda nao bar ya ukweli ni beer mbili anaangusha gari ukimuuliza utasikia oooh jana niliwaka sana