Sunday, November 21
TAMKO LA VIJANA WASOMI WA VYUO VIKUU WA MKOA WA DODOMA, KUHUSU KITENDO CHA BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA KUTOKA NJE YA UKUMBI WA BUNGE.
NDUGU WAANDISHI WA HABARI, NDUGU WANANCHI,.
wali ya yote nawashukuru sana kuhitikia wito wetu wa gfafla kuja kujumika pamoja nasi leo hii, akhsanteni sana.
Sisi vijana wasomi wa vyuo vikuu mbalimbali vilivyoko mkoa wa Dodoma kwa pamoja tunapenda kuweka wazi maoni yetu juu ya kitendo kilichofanywa na Wabunge wa CHADEMA jana 18.11.2010 wakati Mhe. Rais alihutubia Bunge.
Kwanza tumeshtushwa na kitendo hicho na kuweka wazi masikitiko yetu kwa kuwa kilichofanyika ni kinyume na matarajio ya wapiga kura waliowachagua waheshimiwa wabunge hao kuwawakilisha ndani ya chombo hicho kikubwa na chenye heshima kubwa ndani na nje ya nchi.
Bunge ni sehemu ya kuwakilisha wananchi kwa hoja chini ya kanuni zilizopo bila kujali itikadi ya chama chochote cha siasa na kazi kubwa ya mbunge ni kuishauri na kuisimamia Serikali kwa niaba ya wananchi waliomchagua au kuwachagua.
Kwa mantiki hiyo basi kama Wabunge hawamtambui Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania maana yake hawana kazi ya kufanya ndani ya Bunge kwani kazi yao kubwa ni kuishauri na kuisimania Serikali sasa kama hawaitambui Serikali hiyo hawana sababu ya kuendelea kuwepo Bungeni.
Pili Baada ya uchaguzi wa Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda, wabunge hao pia walinukuliwa na vyombo vya habari na ushaidi tunao wakiweka wazi kumkubali kiongozi huyo, na kauli mbiu yake ya ‘Bunge moja’ je, kitendo walichofanya inaashiria utekelezaji wa kauli mbiu ya Bunge moja?
Tatu msimamo wa kutomtambua Rais ni wa CHADEMA kama chama na waliotoka nje ya Bunge ni wabunge sasa ni vema wabune hao watambue na kutafakari upya kama kweli wanawawakilisha Bungeni wananchi au cha na kutekeleza misimamo yao bila kujali maslahi ya waliowachagua na kumpa kura nyingi Rais Kikwete?.
Nne Kwa badhi ya wabunge wa CHADEMA kutomtambua Rais wakati akilihutubia bunge ni wazi kuwa hata sheria zitakzopitishwa na Bunge hawatahusika kwa kuwa mwenye mamlaka ya mwisho kukubali sheria iliyotungwa na Bunge itumike ni Rais ambaye wanadai hawamtutambui.
Ni dhahiri kuwa watashindwa kufanya kazi yao ya uwakilishi na usimamizi wa Serikali Bungeni .
Je wanawaonesha watanzania dalili gani kama si kutaka kuleta machafuko nchini na mgawanyiko ndani ya Bunge na kwa Jamii kwa ujumla?.
Wananchi waliowachagua wabunge hao wanapaswa kutafakari upya wawakilishi waliowachagua kama wana uelewa wa kutosha kuhusu bunge, sisi vijana wa vyuo vikuu tunajua na tunatambua kuwa Rais ni Sehemu ya Bunge na Bunge haliwezi kukamilika bila Rais na hii ndio maana kila sheria inayopitishwa na Bunge ni lazima yeye Rais aweke sahihi yake.
Katika mazungumo yake na waandishi wa habari wiki hii Mweneykiti wa CHADEMA MHE. Freeman Mbowe, alinukuliwa na vyombo vya habari akisema wabunge wake na madiwani wanaweza kuendelea kuwakilisha wananchi licha ya kutomtambua Rais.
Sisi tunasema hili si sahihi bali ni upotoshaji mkubwa, kamwe mtoto hawezi kudai kuwa hamtabui Baba yake kisha anaendelea kumwita Baba na kutumia kila kitu kinachotolewa na Baba huyo huyo. Huo ni utovu wa nidhamu au kukosa maadili.
Sisi vijana wa vyuo vikuu Mkoa wa Dodoma tunawaomba Watanzania wote wenye nia njema na Taifa letu kuwapuuza wabunge wa CHADEMA na kutambua kuwa lengo lao ni kutaka kutuhamisha kutoka kwenye ajenda ya msingi ya Maendeleo na kubaki kwenye malumbano ya kisiasa kama tulivyoshuhudia katika nchi jirani.
Kamwe tusikubali kudanganywa na watu wachache.
Mwisho tungependa kuwaomba Wabunge wa CHADEMA wawaombe radhi watanzania kwa kuvuruga tashwira safi ya Bunge letu lisilo na ubaguzi na itikadi za kisiasa vinginevyo wanawadharau watanzania waliowachagua wakidhani kwamba niwaadilifu wa Taifa na si cha chama chao.
Tutambue kuwa kazi kubwa ya CHADEMA na Wabunge wake kwa sasa ni kuwachanganya watanzania ili badala ya kuendelea na shughuli za ujenzi wa taifa wabaki na malumbano ya hapa na pale kwa manufaa yao binafsi.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Bunge letu na kutuepusha na ubaguzi kama huu uliofanywa na baadhi ya Wabunge wa CHADEMA.
Aksanteni sana.
IMESOMWA NA THOBIAS MWESIGA RICHARD
KWA NIABA YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU MKOA WA DODOMA