I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Thursday, November 25

Mwakyembe ashangaa kocha kumpanga ktkt ..amuuliza kocha nifunge wapi?..kocha akamjibu popote...

SIASA ni mchezo mgumu. Kama ilivyo katika kandanda, aliye nje anayaona makosa, mengi. Walio uwanjani wanaujua uchungu wa game.

Jana nimemwona JK akitangaza baraza lake, si JK wa siku zote. Alikunja uso mara kwa mara. Kuna aliowakunjia uso. Wanasema; kumkoma nyani giladi. Ukitaka kumwua nyani usimtazame usoni.

Sura mpya zilikuwa nyingi. Majina mapya. Kuna majina aliyataja huku akionyesha kuwa anaowataja si watu wake wa karibu. Hakukuwa na ’ mtani wangu nanihii!’

Kama kocha, kikosi kile kinaweza kufanya maajabu. Chaweza kuwa kikosi cha kujituma, maana, wengi waliongizwa kikosini ni wapya. Wanajua nje kwenye benchi kuna wapya wengine, kuna wazoefu. Wakiboronga mchezo, kuna watazamaji watakaopiga kelele majukwaani; ” JK mwingize nanihii!, Mwingize nanihii!”. Ndio mchezo wa siasa ulivyo, kama kandanda vile, kocha ana kazi ngumu, na walio uwanjani pia.

Habari kubwa jana; Samwel Sitta na Harrison Mwakyembe. Kwanini JK amemchezesha Harry Mwakyembe katikati pamoja na akina Jo’ Magufuli na Anna Tibaijuka? Huenda hata Mwakyembe mwenyewe ameshangaa kocha kumpanga katikati. Na labda ameuliza; ” Kocha nifunge wapi?”

JK atamjibu; ” Funga Kote Kote! Anampima akili yake? Na Kwanini Sam Sitta katupwa wingi ya kulia? Nahofia, Sitta ataisubiri sana mipira. Mingi itaishia katikati, hataipata! Ni lazima afanye jitihada binafsi kuitafuta mipira. Na kuna watazamaji jukwaani wanaofikiri, kuwa ingekuwa busara Sam Sitta angechagua kukaa kwenye benchi kulinda heshima yake.
Wanaosema hivyo hawaujui ugumu wa mchezo wa siasa. Sitta atalazimika Ku- ’Like The Situation’ - Kuipenda Hali, basi. Masikini Samwel Sitta, si huyu aliyekuwa na mhimili wake wa dola aliokuwa akiuongoza.

Na ni Sitta huyu huyu aliyepata kutamka bungeni; ” Wapinzani mtaitwa hivyo hivyo, wapinzani, maana nyie mnapinga-pinga tu!”. Alimjibu aliyekuwa Kiongozi wa upinzani Bungeni Hamad Rashid aliyesema kuwa wakati umefika kwa kambi ya Upinzani kuitwa ’ Kambi ya Ushindani’ ili kuondoa dhana ya upinzani ambayo jamii inaitafsiri vibaya.

Masikini Sitta, akiwa Spika wa Bunge alikuwa na nafasi ya kuacha legacy ya kuwezesha hoja ya Watanzania kupata Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ijadiliwe bungeni. Ndio, Samwel Sitta sasa atakumbukwa pia kwa kuwa Spika wa kwanza kujenga ofisi yake ya Spika kwao Urambo Mashariki. Ofisi yenye thamani ya mamilioni ya fedha za walipa kodi. Hivi alidhani Uspika ni Usultani?!

Naam. Na kwenye mchezo mgumu wa siasa kuna kinachoitwa ’ Inner cabinet’. Kikundi kidogo cha mawaziri kinachoweza kukutana na Rais hata isipo rasmi. Kitapanga mikakati kabla ya kukutana na baraza zima. Kama kuna ’ Inner Cainet’ pale Magogoni, basi, sina hakika kama Sam Sitta na Harry Mwakyembe watakuwamo. Si ni juzi tu walikuwa ’ a political loose cannons’ ndani ya chama- Mizinga inayoning’inia, inapiga Kote Kote! Na bado ndani ya chama kuna hofu ya uwepo wa masalia ya ’ Weapons Of Mass Political Destructions’. Anne Kilango, Ole Sendeka.....

Naam. Katika miaka ya karibuni, inaaminika kuwa Bungeni Sitta aliipa tabu sana Serikali. Bado hatujaandika, na itakuja, simulizi ya ’ Mitume 12’ iliyopambana na ufisadi ndani na nje ya bunge. Samwel Sitta alikuwa mmoja wa mitume hiyo. Harry Mwakyembe nae alikuwamo. Hawakujua kuwa, ni kazi ngumu sana kupambana na ufisadi kwa kelele za bungeni tu. Dawa ni Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi. Ndio, tatizo ni MFUMO uliopo ambao nao walikuwa ni sehemu ya mfumo huo.
Katika mchezo wa siasa; adui yako usimwache nje ya hema akunanilihii haja ndogo ukiwa ndani ya hema. Mwingize ndani ya hema ananilihii haja ndogo nje akiwa ndani ya hema.

Naam.Wanaosema siasa ni mchezo mchafu wanakosea. Siasa ni mchezo mgumu, basi.

Na Maggid, Iringa Novemba 25, 2010