I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Monday, November 1

BREAKING NYUUUUUZZZZZZZ: DK. ALI MOHAMED SHEIN ASHINDA UCHAGUZI ZANZIBAR


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bw. Khatib Mwinyichande akitangaza matokeo ya urais Zanzibar katika hoteli ya Bwawani mjini Unguja usiku huu
Rais mteule wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein akitoa
shukrani baada ya kutangazwa mshindi

Mgombea urais wa Chama cha Wananchi CUF
Maalim Seif Shariff Hamad akikubali matokeo

MGOMBEA WA CCM KATIKA KUGOMBEA URAIS WA ZANZIBAR DK. ALI MOHAMED SHEIN AMESHINDA URAIS ZANZIBAR KWA MUJIBU WA MATOKEO YA TUME YA UCHAGUZI SASA HIVI KWA ASILIMIA 66.4%

MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AKUBALI MATOKEO NA KUIPONGEZA CCM NA MGOMBEA WAKE. ANAHUTUBIA HIVI SASA NA KUMKUBALI DK. ALI MOHAMED SHEIN KWA KUPATA RIDHAA YA WAZANZIBARI KUWAONGOZA KWA MIAKA 5 IJAYO AKIWA RAIS WA AWAMU YA SABA VISIWANI HUMO.

HATA HIVYO MAALIM SEIF AMESEMA KUNA DOSARI ZINAZOTOKANA NA BADHI YA MAOFISA NA KUMUOMBA RAIS MTEULE KUWA MWANGALIFU NA HILO ILI NCHI ISIFIKE PABAYA.

AMESEMA KATIKA UCHAGUZI HUU HAKUNA MSHINDI AMA MSHINDWA. MSHINDI NI MZANZIBARI. NA KAMUOMBA RAIS MTEULE AHAKIKISHE HILO ILI HALI YA HEWA ISIJE KUCHAFUKA. ANAMALIZA HOTUBA NA KWENDA KUMPA MKONO DK. SHEIN HUKU VIFIJO NA NDEREMO VIKIUMUKA KATIKA KILE KILICHOITWA MATUMAINI MAPYA KWA ZANZIBAR.

DK. SHEIN ANAITWA KUONGEA SASA.ANAINUKA NA KUELEKEA KWENYE KIPAZA SAUTI. UKUMBI UMEJAA MSISIMKO SI WA KAWAIDA. ANAMFAGILIA MAALIM SEIF KWA HOTUBA FUPI LAKINI NZITO, ANAAHIDI KUSIMAMIA VYEMA UUNDAJI NA UENDESHAJI WA SERIKALI YA MSETO NA KUKUBALIANA NA MAALIM SEIF KUWA HAKUNA MSHINDI ILA WAZANZIBARI WOTE KWA MUSTAKABALI WA MAENDELEO YA VISIWANI.

GLOBU YA JAMII INAMPONGEZA
DK. MOHAMED ALI SHEIN KWA USHINDI HUU WA KIHISTORIA.

VIDEO YA TUKIO HILI INAANDALIWA. TUVUTE SUBIRA........
TUKIO HILI LINARUSHWA LIVE NA TBC ONE