I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Monday, March 1

HOTUBA YA JK YA MWISHO WA MWEZI WA FEBRUARI 2010


HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI YA MWISHO WA MWEZI FEBRUARI, 2010

Ndugu Wananchi, Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetuwezesha kukutana kwa mara nyingine tena na kuzungumza kwa mujibu wa utaratibu wetu mzuri wa kuzungumza kila mwisho wa mwezi.

Mwisho wa mwezi uliopita hatukuweza kuzungumza kwa sababu nilikuwa Addis Ababa, Ethiopia kwenye mkutano wa kila mwaka wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika. Hata hivyo niliitumia fursa ya hotuba yangu katika Sherehe za Miaka 33 ya CCM tarehe 6 Februari, 2010 kuzungumzia baadhi ya masuala muhimu kitaifa.

Siku ya leo nataka kuzungumzia jambo moja tu, nalo ni Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi uliopitishwa na Bunge letu tukufu katika kikao chake kilichopita. Hivi karibuni nitatia saini muswada huo kuwa Sheria.

Kwa sasa matayarisho ya shughuli hiyo yanaendelea. Ndugu Wananchi; Chimbuko la kutungwa sheria hii ni mwenendo usiyoridhisha wa matumizi ya fedha katika chaguzi zetu nchini. Kuna matumizi mabaya ya fedha katika uchaguzi ndani ya vyama vya siasa na baina ya vyama vya siasa katika chaguzi za kiserikali.

Katika hotuba yangu ya kuzindua Bunge tarehe 30 Desemba, 2005, nilizungumzia kutokuridhishwa kwangu na hali hii na nilielezea nia yangu ya dhati ya kutaka kuchukua hatua thabiti za kuweka utaratibu utakaoongoza na kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi. Naomba ninukuu maneno niliyosema siku ile: “Jambo lingine linalonisumbua linahusu upatikanaji na matumizi ya fedha na michango mingine kwenye Uchaguzi.

Yameanza kujitokeza mawazo, pamoja na kuanza kujengeka utamaduni kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa fedha. [............] tusipokuwa waangalifu nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo.

Ni kweli kwamba fedha ni nyenzo mojawapo muhimu katika kufanikisha uchaguzi, kwa kila chama na kwa kila mgombea. Lakini, fedha kutumika kununua ushindi si halali. Kwa maoni yangu hatuna budi kupiga vita utamaduni huu kwa nguvu zetu zote. Ni vema sasa tuanzishe mjadala wa kitaifa na hatimaye kuelewana kuhusu utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutafuta fedha za uchaguzi; na utaratibu halali ulio wazi, wa chama au mgombea kutumia fedha hizo. Na utaratibu tutakaokubaliana uwe ni sehemu ya maadili ya uchaguzi katika uchaguzi wa kiSerikali na ndani ya vyama vya Siasa.” Mwisho wa kunukuu.

Ndugu wananchi, Jambo hili tumekuwa tunalifanyia kazi Serikalini tangu tuingie madarakani. Kwa vile ni jambo jipya na kwa nia ya kuepuka kuanza vibaya, tumefanya utafiti wa kutosha na kujifunza kutoka mifano ya nchi ambazo zina utaratibu wa aina hii. Kadhalika, hapa nchini, tuliwahusisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, asasi zisizo za kiserikali, Tume ya Uchaguzi, Msajili wa Vyama vya Siasa na watu wengine wengi.

Ndugu Wananchi; Matokeo ya kazi hiyo nzuri ni kutengenezwa kwa Muswada wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi ambao uliwasilishwa katika kikao kilichopita cha Bunge kwa uamuzi. Kabla ya kupelekwa Bungeni, rasimu ya Muswada huu ilijadiliwa kwa kina Serikalini.

Pale Dodoma Bungeni, muswada huu ulijadiliwa kwa siku kadhaa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala na kwenye vikao vya Kamati za Vyama vya Siasa. Katika jamii nako, Muswada huu uliibua mijadala iliyokuwa na hisia za namna mbalimbali na wakati mwingine mijadala hiyo ilikuwa mikali. Kwa ujumla, mijadala yote hiyo ilisaidia kuboresha maudhui ya Muswada na hatimaye kupata ule uliopitishwa na Bunge letu Tukufu tarehe 11 Februari, 2010.

Ndugu Wananchi; Tumetunga Sheria hii mpya kwa nia ya kupata majawabu kwa tatizo la matumizi mabaya ya fedha katika shughuli za uchaguzi. Tunatambua kuwa matatizo haya si mageni, yamekuwepo tangu miaka mingi huko nyuma na hata historia ya Bunge letu ina ushahidi wa ushindi wa baadhi ya Wabunge kutenguliwa kwa makosa ya rushwa. Lakini, siku hizi matatizo ya matumizi mabaya ya fedha yamekuwa makubwa zaidi na yanakua kwa kasi inayotishia kugeuzwa kuwa ndiyo utaratibu wa kawaida au utamaduni katika chaguzi zetu. Ni hali ambayo haifai kuachwa kuendelea na kuzoeleka. Hatuna budi kuchukua hatua za dhati kurekebisha mambo na kulirejesha taifa katika mstari ulionyooka.

Ndugu Wananchi; Tuliamua kuwa, hatua muafaka ya kuchukua ni hii ya kutunga sheria ya kuongoza na kudhibiti matumizi ya fedha katika uchaguzi. Sheria hii ikitekelezwa ipasavyo itazuia kugeuza uongozi kuwa ni kitu cha kununuliwa kama bidhaa na wenye pesa au wanaoweza kupata pesa za kufanya hivyo. Aidha, itakomesha kabisa tabia mbaya inayoanza kujitokeza ya wapiga kura kugeuza kura yao kama bidhaa ya kuchuuza kwa wagombea.

Misingi ya Sheria
Ndugu Wananchi, Katika kufikiria na kutayarisha rasimu ya muswada wa sheria hii, mambo saba ya msingi yalizingatiwa. Mambo hayo ni haya yafuatayo: Kuutambua kisheria mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama vya siasa na kuusimamia kisheria. Kuweka utaratibu wa kisheria utakaosimamia na kuratibu mapato na kudhibiti matumizi pamoja na gharama za uchaguzi kwa vyama vya siasa na wagombea. Kuweka viwango kwa matumizi na gharama za uchaguzi.

Kuweka utaratibu utakaosimamia mapato na matumizi ya vyama vya siasa ikiwa ni pamoja na zawadi, misaada na michango itakayotolewa na wagombea au wahisani wakati wa kampeni za uchaguzi. Kudhibiti michango na zawadi kutoka nje ya nchi.

Kuweka utaratibu na mfumo wa udhibiti na uwajibikaji kwa mapato na matumizi ya fedha za uchaguzi kwa upande wa vyama vya siasa na wagombea. Kuainisha adhabu kwa watakaokiuka masharti yatakayowekwa na Sheria hii. Uteuzi Ndani ya Vyama Umetambuliwa

Ndugu Wananchi, Katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi, mambo yote hayo ya msingi yamezingatiwa. Ni Sheria inayojitosheleza kwa kila hali pamoja na ukweli kwamba ni mara ya kwanza tunakuwa na sheria ya namna hii. Sheria yetu mpya imezitambua rasmi gharama zinazotumika na vyama vya siasa na wagombea kuanzia wakati wa mchakato wa uteuzi ndani ya vyama mpaka wakati wa uchaguzi wenyewe.

Sheria hii sasa inafafanua gharama za uchaguzi kuwa ni zile zinazotumika na Vyama, Wagombea au Serikali wakati wa uteuzi ndani ya vyama, wakati wa uteuzi kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, wakati wa kampeni na hadi siku ya kupiga kura.

Ndugu Wananchi; Kabla ya Sheria hii kutungwa, matumizi mabaya ya fedha wakati wa uteuzi wa wagombea katika vyama vya siasa yalionekana kuwa ni matatizo ya ndani ya vyama husika, hivyo yaliachiwa vyama vyenyewe kushughulika nayo wajuavyo. Kwa mujibu wa Sheria yetu mpya mchakato wa uteuzi wa wagombea ndani ya vyama umetambuliwa rasmi kuwa ni sehemu kamili ya uchaguzi, hivyo matumizi ya fedha ya vyama na wagombea yametengezewa utaratibu wa udhibiti.

Kwa hiyo, kuanzia sasa kuhonga au kuhongwa katika mchakato wa uteuzi ndani ya vyama kutamulikwa kwa karibu na wahusika wataadhibiwa na vyombo vya dola.

Uwazi wa Mapato na Matumizi

Ndugu Wananchi; Jambo lingine muhimu katika Sheria hii ni kwamba, inaweka sharti la uwazi katika mapato na matumizi ya vyama na wagombea kwa ajili ya uchaguzi kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Sheria pia inaelekeza utaratibu wa kufuatwa na vyama na wagombea katika kutoa taarifa zao za mapato na matumizi ya uchaguzi.

Kila mgombea, kwa mfano, atatakiwa kutoa kabla ya uchaguzi, taarifa ya fedha alizonazo na makisio ya fedha anazotarajia kupata kwa ajili ya kampeni na uchaguzi, ndani ya siku saba (7) baada ya uteuzi wa wagombea kufanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Baada ya uchaguzi atatakiwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi halisi siku tisini (90) baada ya matokeo kutangazwa. Ndugu Wananchi; Vyama vya siasa, navyo hali kadhalika, vitatakiwa kutoa taarifa ya mapato yao pamoja na makisio ya mapato wanayotegemea kuyapata kwa ajili ya gharama za uchaguzi kabla ya uteuzi wa wagombea.

Baada ya uchaguzi, vyama hivyo vinatakiwa vitoe taarifa ya mapato na matumizi yake halisi ndani ya siku tisini (90) baada ya matokeo rasmi ya uchaguzi kutangazwa.

Taarifa hizo za vyama na wagombea zinatakiwa zionyeshe wazi vyanzo vyote vya mapato ikiwemo michango ya fedha na mali (vifaa, zana, magari n.k.), pamoja na mchanganuo wa matumizi yake. Uwazi wa Michango Ndugu Wananchi, Kwa upande wa michango ya hiyari na zawadi zinazotolewa kwa Chama na wagombea, Sheria inataka pawepo na uwazi katika utoaji wake.

Sheria inaelekeza kwamba, kila chama cha siasa kilichopokea mchango unaozidi shilingi milioni moja kutoka kwa kila mchangiaji binafsi au shilingi milioni mbili kutoka kwa taasisi, kitoe taarifa kwa Msajili.

Aidha, Sheria inataka fedha hizo zihifadhiwe katika akaunti maalum itakayofunguliwa kwa ajili hiyo. Fedha hizo zitalipwa na kutumika kutoka katika akaunti hiyo. Naomba ieleweke kuwa, si nia ya Sheria hii kuzuia wananchi kuchangia shughuli za siasa au za kampeni za Chama wakipendacho au mgombea wanayempenda. Sheria inaruhusu michango ya aina yoyote kutolewa kwa chama chochote au kwa mgombea yeyote ila inataka michango hiyo itolewe kwa utaratibu ulio wazi. Kusiwe na usiri au kificho cha namna yoyote.

Ndugu Wananchi; Sheria pia inafafanua utaratibu wa vyama au wagombea kupata misaada kutoka nje ya nchi. Sheria inazuia michango na misaada hii isitolewe wakati wa kampeni. Inaruhusu vyama vya siasa au wagombea kupokea misaada kutoka nje ya nchi siku 90 kabla ya Uchaguzi Mkuu au siku 30 kabla ya uchaguzi mdogo.


Pia, inataka kuwepo uwazi na taarifa itolewe kwa Msajili wa Vyama vya Siasa. Najua suala la masharti yaliyowekwa kwa watu wa nje kuchangia vyama vya siasa na wagombea nchini lilizua mjadala miongoni mwa wadau mbalimbali. Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa baadhi ya vyama vya siasa kupinga masharti yaliyowekwa. Naomba ieleweke kuwa, kwa kweli, si jambo jema kwa Chama cha siasa au mgombea nchini kufadhiliwa na watu wa nje. Wahenga wanasema “anayemlipa mpiga zumari huchagua wimbo”.


Ipo hatari kwa kiongozi au chama kupokea amri kutoka nchi za nje kwa kuwasikiliza wale watu wa nje waliowasaidia badala ya kujali maslahi ya nchi yetu na watu wake.

Uwajibikaji Kuhusu Michango
Ndugu Wananchi, Sheria pia inaweka sharti la uwajibikaji wa vyama vya siasa, wagombea na washiriki wengine kuhusu michango, mapato na matumizi katika uchaguzi. Sheria inaelekeza kwamba:- Kila mchango unaopokelewa na matumizi yatakayofanyika kwa ajili ya uchaguzi vifanywe na Chama na siyo vinginevyo. Chama cha siasa kitawajibika kwa matumizi yote yatakayofanywa na chama au wagombea wake, na kwamba matumizi yote yanatakiwa kuwa na risiti. Kila mgombea atawekewa mgawo wake wa matumizi ya kampeni na chama kitatoa taarifa ya fedha iliyokaguliwa kwa matumizi hayo.

Chama kitakachoshindwa kutunza taarifa hizo kitakuwa kimetenda kosa na kitastahili adhabu. Kila mgombea atakayepokea mchango atapaswa kutoa taarifa kwa chama chake kuhusu mapato na matumizi yanayohusu mchango huo. Kila chama cha siasa, taasisi ya kiraia, taasisi ya kidini au taasisi ya kijamii itakayohusika katika kuchangia shughuli za uchaguzi, inayo wajibu wa kutunza taarifa za fedha zinazoelezea mapato na matumizi yao.

Mambo haya ni muhimu sana kwani bila ya kuwepo utaratibu wa uwajibikaji kwa upande wa wahusika, Sheria yote itakuwa haina maana. Matatizo tunayojaribu kuyapatia ufumbuzi yatakuwa hayakushughulikiwa ipasavyo. Mambo Yaliyokatazwa Ndugu Wananchi; Sheria imeainisha vizuri mambo yanavyokatazwa kwa upande wa matumizi ya fedha za uchaguzi.

Sheria inakataza, kwa mfano, vitendo vifuatavyo visifanyike pamoja na matumizi ya fedha kwa ajili hiyo kuzuiliwa:

*Kufanya malipo kwa wapiga kura ili wamchague mgombea fulani; Kuahidi kazi au cheo au wadhifa kwa mpiga kura ili amchague mgombea;

*Kutoa zawadi, ahadi, mkopo, au makubaliano yoyote kwa mpiga kura ili amchague mgombea; Kukubali kurubuniwa kwa mambo yoyote yaliyotajwa hapo juu ili ampigie kura mgombea yeyote;

*Kufanya vitendo vyovyote kati ya hivyo wakati wowote kabla au hata baada ya uteuzi wa mgombea;

*Kutoa malipo kwa ajili ya takrima ya chakula, vinywaji au starehe yoyote kwa ajili ya kuwashawishi wapiga kura wamchague mgombea;

*Kuwasafirisha wapiga kura ili wamchague mgombea.

Hata hivyo Sheria inaruhusu wapiga kura wenyewe kujilipia nauli kwenda kupiga kura au Serikali kuwasafirisha wapiga kura pale ambapo kuna shida ya usafiri;
Kuweka mkataba wowote ule wa pango kwa niaba ya wapiga kura ili wamchague mgombea; Chama au mgombea au mtu yeyote atakayetenda vitendo hivi nilivyovitaja atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii na ataadhibiwa ipasavyo. Viwango vya Gharama za Uchaguzi

Ndugu Wananchi, Sheria ya Gharama za Uchaguzi inaweka utaratibu wa kudhibiti gharama za uchaguzi kwa kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya uchaguzi kuweka viwango vya gharama za uchaguzi.

Waziri huyo atatangaza kiwango cha juu ambacho kila mgombea ataweza kutumia katika kampeni na katika uchaguzi. Kiwango hicho cha gharama kitazingatia tofauti ya majimbo, idadi ya watu, aina ya wagombea pamoja na miundombinu.


Chama au mgombea atakayevuka viwango vya mtumizi alivyowekewa bila maelezo ya kuridhisha, atakuwa ametenda kosa na anastahili kuwajibishwa ipasavyo.


Utaratibu huu ni muhimu katika kujenga nidhamu na usawa miongoni mwa vyama na wagombea katika uchaguzi. Hivi sasa kwa sababu ya kutokuwepo ukomo, wako watu wenye pesa ambao wanafanya matumizi kupita kiasi. Wapo wanaopitiliza au hata kukufuru na kuwadhalilisha wenzi wao wasiokuwa na uwezo kama wao.


Ndugu Wananchi, Mimi naamini, hatua zilizomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi zikitekelezwa, zitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au hata kudhibiti kabisa vitendo na hisia za rushwa katika uchaguzi.


Mara nyingi vitendo hivyo vinapofanyika, au hata kule kuwepo hisia tu kwamba vinaweza kuwa vimefanyika, huwa ni chanzo cha manung’uniko na kukosekana utulivu. Wakati mwingine huathiri taswira ya demokrasia yetu na heshima ya uongozi uliochaguliwa hasa pale uhalali wa matokeo ya uchaguzi unapotiliwa shaka.


Tunachukua hatua hizi ili kulinda hadhi ya chaguzi zetu nchini na kuzifanya kweli ziwe huru na za haki na kufanya mfumo wa demokrasia uzidi kustawi. Hatima ya yote haya tufanyayo ni kusaidia nchi yetu kuwa na viongozi wanaotokana na ridhaa ya wananchi.

Ndugu zangu; Demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu bado ni changa. Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa nne tangu turudi kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992. Ni muhimu sana, mapema kabisa, kuchukua hatua thabiti za kuilinda demokrasia yetu hii na kuhakikisha inakua na kujengeka katika misingi iliyo sahihi. Sheria hii mpya, tukiisimamia vizuri na kuitekeleza itafanikisha azma yetu hiyo.

Tutakuwa tumepiga hatua kubwa katika maendeleo na ustawi wa demokrasia nchini. Mafanikio ya dhamira yetu njema yanategemea sana utashi na ushirikiano wa viongozi na wanachama wa vyama vya siasa pamoja na wananchi katika utekelezaji. Ni matumaini yangu kwamba viongozi wenzangu wa siasa tutaipokea kwa moyo mkunjufu na kuiunga mkono Sheria hii mpya.

Ni matumaini yangu pia kwamba, sisi viongozi tutawahamasisha wanachama wetu, wapenzi wa vyama vyetu na wananchi wenzetu kwa jumla kuzingatia na kutekeleza Sheria hii. Ndugu Zangu,

Wananchi Wenzangu, Nimetumia muda wenu mwingi kuwadokeza baadhi ya mambo ya msingi yaliyomo katika Sheria ya Gharama za Uchaguzi. Nia yangu ni kufanya mambo matatu muhimu.

Kwanza, kuwathibitishia Watanzania wenzangu kwamba tunalitambua tatizo la rushwa katika uchaguzi na tunayo dhamira ya dhati ya kupambana nalo. Kukemea peke yake hakutoshi, lazima tutumie nguvu ya sheria kudhibiti vitendo vya rushwa na kuwaadhibu ipasavyo wahusika.



Pili, kuwathibitishia kuwa sisi wenzenu tuliopo katika Serikali tunatambua wajibu wetu wa kuhakikisha kuwa Sheria hii inatekelezwa kwa ukamilifu. Nimekwishaviagiza vyombo vya dola, ikiwemo TAKUKURU, kujipanga vizuri kuisimamia Sheria hii na kuwabana ipasavyo wale wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuanzia katika uchaguzi wa mwaka huu. Nawaomba wananchi mtoe ushirikiano kwa vyombo vyote vinavyohusika na usimamizi wa Sheria hii ili vitimize kwa ukamilifu malengo yake ambayo yana maslahi kwa nchi yetu na kwetu sote.



Tatu, napenda kuwaambia kwamba, sisi katika Serikali tunatambua wajibu wa kuhakikisha kuwa wananchi, wanachama na viongozi wa vyama vya siasa wanaelimishwa vya kutosha ili waielewe vizuri Sheria hii. Umuhimu wa kuielewa vizuri Sheria hii hauhitaji kusisitizwa kwani watu wakiielewa vizuri inarahisisha utekelezaji wake.


Na, kwa vyama vya siasa na wagombea, uelewa mzuri utasaidia kuepuka makosa ambayo yanaweza kuwa na gharama kubwa ya wao kupoteza ushindi. Natambua kwamba Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Ofisi ya Waziri Mkuu wanajiandaa vizuri kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu maudhui ya Sheria hii muhimu.



Nawaomba ndugu wananchi tusikilize kwa makini ufafanuzi watakaoutoa kwa manufaa yetu na ya nchi yetu.


Ndugu Wananchi; Naomba nimalize hotuba yangu kwa kuwashukuru kwa mara nyingine tena kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali yetu. Naomba tuendelee kushirikiana katika utekelezaji wa Sheria hii muhimu kwa ajili ya kukuza na kuendeleza demokrasia katika nchi yetu.


Nataka kuona katika chaguzi zetu nchini tunajenga utamaduni wa kushindanisha sera za vyama na uwezo wa wagombea kuliko kushindanisha uwezo wa kukusanya fedha za kampeni.

Asanteni kwa kunisikiliza!
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania

Sunday, February 28

check out these clips

Thursday, February 18

CHIZIKA NA Tanzania - Swahili Bongo Flava



JIDE ASHINDWA KUSIMAMA



Ripoti ya uchunguzi wa Ijumaa inakwenda mbele zaidi ya ugonjwa wa Malaria ambao hivi karibuni ulimlazimu kukimbizwa kwenye hospitali daraja la kwanza Dar, Aga Khan baada ya kukumbwa na tatizo la mwili kuishiwa nguvu na kushindwa kutembea.

Ijumaa limebaini kuwa, Jide hapati muda wa kupumzika kutokana na ratiba yake kuwa ‘taiti’ hivyo kuulazimisha mwili wake kupiga mzigo bila kujali uchovu.

Aidha, kuna ‘nyiuzi’ za kidaku kuwa, kufuatia kuwa ‘taiti’ kupita maelezo akipanda majukwaani na bendi yake ya Machozi kutoa burudani, mwanamuziki huyo amekuwa akikumbwa na uchovu mkubwa kupita kiasi hivyo mwili kuwa katika hali ya kudhoofu na wakati mwingine kushindwa kusimama kwa muda mrefu.

CHILL OUT WITH THIS CLIP BY RIHANNA rude boy

Saturday, February 13

HISTORY OF VALENTINE'S DAY










Valentine's Day is a holiday that happens on February 14. It is the day of the year when lovers show their love to each other. This can be done by giving flowers, chocolates or Valentine's cards. Love notes can be given to one another. These notes are called valentines. Symbols of Valentine's Day are heart shapes, roses, and Cupid with his arrows. Valentine's Day is named for two martyred Christian saints named Valentine. Since the 15th century Valentine's pairs are formed in England. English emigrants took the Valentine's custom to the United States. After theSecond World War, US soldiers brought this festival to Europe.

Legend

In the third century after Christ, Valentine was the bishop of Terni (Italy). He performed weddings for couples who were not allowed to get married. They may not have been allowed to get married because the parents did not agree with the connection or because the bridegroom was a soldier or a slave, so the marriage was forbidden. Valentine gave to the married pairsflowers from his garden. That's why flowers play a very important role on Valentine's Day. This did not please the emperor. On February 14, 269 AD, Valentin was beheaded because of hisChristian faith. An expansion of the legend combines the day of death of Valentine with the Roman festival Lupercalia. It was the festival of the great goddess Lupa, which is the feminine word for wolf. She was the Great She-Wolf who nursed the twin babies, Romulus and Remus, who later became the founders of Rome. During the annual ceremony, the temple priestesses (lupae) wrote their names on strips of papyrus. These were picked by young men. After the lottery, the youngsters walked through the city and got the blessings of the citizens. The martyr Valentine became the patron saint of the lovers. Still in the Middle Ages, as in France or in Belgium, people were chosen by the lottery to live a year with each other and people prayed to Saint Valentin to make love potions and charms. United States and Europe In the 19th century, the custom of sending Valentine's Cards became very popular. The cards usually have pictures of hearts or flowers and contain some sort of poem, message, or code. Codes and simple messages give some people the courage to show their true feelings to the person they love. Today, some people still use mysterious codes to show their love. People can use newspapers to give a coded message to their loved one, giving other readers a view of the couples' intimacy with one another. Famous for the popularity of the celebration is the folk song called "Die Vogelhochzeit" ("The Birds' Wedding"). China In China, a holiday called Qi Xi is also called "Chinese Valentine's Day", especially by younger people. Qi Xi is traditionally held on the 7th day of the 7th month of the lunar calendar. In recent years, it has become more like Valentine's Day in other countries.

Wednesday, February 10

TSAH IMEAANDAA SAFARI YA VALENTINE ITAKAYOFANYIKA HAPA AALANKRITA RESORT

Safari itaanza saa tatu na nusu asubuhi jumapili tarehe 14th feb 2010 kuelekea Aalankrita resort, maeneo haya unayoyaona katika pics,ambapo watu watashangweka mpaka kuche.wanajumuiya wote mnakaribishwa,...vinywaji vya aina zote vitakuwepo,musik,swimming pool, lunch ya pamoja,dina na mengine mengi.........
yote hayo yanapatikana kwa mchango wa rupees 700/= tu.
Njoo ushangweke na watanzania wenzako wa hyderabad,jiliwaze na watz wenzako.

hawa ndio wakusanyaji wa michango kwa wanaoishi sainikpuri wamuone DANI ,singapuri,FLAVIANA na LISA, tolichowki MATATA NA M/KITI,nampally MUUMINI pia unaweza kuonana na watu wa kamati ya fedha tsah kama vile muweka hazina
more inf; call 9963702460 or 9703250802







Tuesday, February 9

HUYU NDIO STARLING WA MITIHANI YA FORM 1V 2009 TANZANIA IMMACULATE MOSHA: THE GENIUS GIRL!


msichana mwenye kipaji aliyeoongoza nchi nzima katika matokea ya mitihani ya kidato cha Nne 2009 Tanzania.

Monday, February 8

RAIS JAKAYA KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MNIKULU RAJABU MOHAMMED KIANDA



Mama Salma Kikwete akimfariji Bi.Khadija Kianda mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa mnikulu kufuatia kifo chake kilichotokea jumapili jijini Dar es Salaam.

akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la aliyekuwa mnikulu Bwana Rajabu Kianda aliyefariki jana jijini Dar es Salaam.Marehemu Kianda anatarajiwa kuzikwa leo (tarehe 9/2/2010) nyumbani kwao Kihurio Same Mkoa wa Kilimanjaro.


akimfariji Bi.Khadija Kianda ambaye ni mjane wa Marehemu Rajabu Kianda aliyekuwa Mnikulu ambaye alifariki dunia Jumapili jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete alikwenda nyumbani kwa marehemu eneo la Mikocheni jijini Dar es Salaam kuifariji familia ya marehemu ambaye anatarajia kuzikwa huko Kihurio Same,Mkoani Kilimanjaro.Pembeni ni Mama wa Marehemu Bi. Mwanahawa Samuel.

MNYIKULU- Hili ni neno la kinyamwezi lilikokuwa likitumiwa wakati ule wa utawala wa kitemi, Mtemi Mirambo wa wanyamwezi alikuwa na wasaidizi wake, hawa walikuwa wakiitwa "Wanyikulu" kwani nyumba ya mtemi ilikuwa ikiitwa "IKULU" sehemu ambapo maamuzi ya vita na mipango yote ya kiutawala inafanyikia. Hivyo basi sisi wanyamwezi tulikuwa tunawaita wasaidizi wa mtemi kuwa ni "WANYIKULU" ambao walikuwa na dhamana ya kuhakikisha mambo yote ya kiutawala yanaenda kama kawaida wakisaidiwa na "MAKATIKILO"-hawa ni kama wajumbe wapeleka habari. hivyo mnikulu ni mtendaji mkuu ikulu ya rais.

MBUZI WA CHINA WANAWEZA KUPANDA MITI NA KUSHUKA KAMA BINADAMU



Mbuzi unaowaona pichani hupatikana nchini MOROCCO, inasemekana ni kawaida kuwaona mbuzi wakiwa wamepanda juu ya vichaka na miti midogo ni kwa sababu wanafuata matunda yajulikanayo kama ARGO, kutokana na kuyapenda sana matunda hayo basi mbuzi hao hudandia juu ya matawi ya vichaka ili kupata matunda hayo.

T.I AKIWA NA MCHUMBA WAKE


T.I.D, TOP IN DAR AKIWA NA MCHUMBA WAKE MARA BAADA YA KUMALIZA SHOW.HAPA KATIKA PICS WAMEKAA MKAO WA KWENDA KUSWALI KUEPUKANA NA MATATIZO MBALIMBALI YANAYOWEZA KUJETOKEZA CKU ZA USONI

ENJOY NA ZE COMEDY SHOW DAR 2 MORO




MATOKEO YA KIDATO CHA NNE TANZANIA SHULE ZA SERIKALI HOI

MATOKEO ya mtihani wa kumaliza kidato cha nne kwa mwaka 2009 yametangazwa jana na Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) huku yakionyesha shule za serikali zikiendelea kufanya vibaya kwa kushindwa kuwemo kwenye shule 10 bora huku kiwango cha ufaulu kikizidi kupungua.

Aidha, matokeo ya mtihani huo uliofanyika Oktoba mwaka jana yanaonyesha kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa asilimia 11.2 kwani mwaka 2008 kilikuwa asilimia 83.69 wakati mwaka huu kikishuka hadi kufikia asilimia 72.51

Akitangaza matokeo hayo jana jijini Dar es salam kwenye ofisi za baraza hilo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk. Joyce Ndalichako, alisema watahiniwa 351,152 walisajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne, kati yao wasichana ni 167,591 sawa na asilimia 47.73 na wavulana 183,561 sawa na asilimia 52.27 wakati mwaka 2008 watahiniwa 241,472 walisajiliwa.

Alibainisha kuwa watahiniwa 42,672 sawa na asilimia 17.85 wamefaulu katika daraja la kwanza hadi la tatu ambapo wasichana ni 13,788 sawa na asilimia 12.47 na wavulana 28,884 sawa na asilimia 22.48.

Alisema, watahiniwa waliopata daraja la nne ni 130,651 sawa na na asilimia 54.66 wakati waliopata sifuri ni 65,708 sawa na asilimi 27.49 idadi inayoonekana kuongezeka tofauti na mwaka jana.

Akizungumzia hilo, Joyce alisema kati ya shule 10 bora hakuna shule ya serikali hata moja na kueleza kwamba shule zinazoongoza ni zile za seminari na nyingine zinazomilikiwa na watu binafsi.

Katibu huyo alizitaja shule 10 bora zenye watahiniwa zaidi ya 35 kuwa ni Shule ya Wasichana Marian na St. Mary’s Junior Seminary, zote za Bagamoyo; St. James Seminary, Uru Seminary, Anwarite Girls, Maua Seminary na St. Mary Goreti, zote za Kilimanjaro; nyingine ni Don Bosco Seminary ya Iringa; St. Francis Girls ya Mbeya; na Feza Boys ya Dar es Salaam.

Aidha, alizitaja shule 10 bora zenye wanafunzi chini ya 35 kuwa ni Feza Girls; Thomas More Machrina na Hellen’s za Dar es Salaam; Mafinga Seminary na Bethelsabs Girls za Iringa; na St. Joseph-Kilocha seminary ya Kilimanjaro.

Nyingine ni Queen of Apostles Ushirombo ya Shinyanga; Dungunyi Seminary ya Singida; Rubya Seminary ya mkoani Kagera; na Sengerema Seminary ya Mwanza.

Alisema nafasi ya kwanza kwa mtahiniwa aliyefanya vizuri imekwenda kwa msichana Imaculate Mosha kutoka Marian Girls wakati mvulana bora ni Gwamaka Njobelo wa Shule ya Sekondari Mzumbe.

Hata hivyo alizitaja shule zilizoshika mkia zenye wanafunzi zaidi ya 35 kuwa ni Sekondari ya Busi na Jangalo za Dodoma; Sekondari ya Misima, Chekelei na Potwe za Tanga; Sekondari ya Milola na Mandawa za Lindi; Sekondari ya Kiwere ya Tabora; Sekondari ya Msata ya Pwani; na Sekondari ya Masanze ya Morogoro.

Sekondari nyingine zilizofanya vibaya zenye wanafunzi chini ya 35 ni Kizara ya Tanga; na Mingumbi, Nahukahuka, Marambo, Ruponda na Mpunyule zote za Lindi. Nyingine ni Songolo ya Dodoma; Dole ya Zanzibar; Ruruma ya Singida; na Viziwi Njombe ya Iringa.

Pamoja na hayo alisema jumla ya watahiniwa 410 wamefutiwa matokeo yao chini ya kifungu namba 52 cha kanuni za mitihani baada ya kubainika kwamba walifanya udanganyifu.

Aliongeza kuwa watahiniwa 184 walibainika kuwa na makaratasi yenye miandiko tofauti au kuwa na miandiko tofauti katika mtihani wa somo; watahiniwa 141 walikamatwa na wasimamizi ndani ya chumba cha mtihani wakiwa makaratasi yanayohisiwa kuwa na majibu ya somo husika.

Alisema kuwa watahiniwa 64 walibainika kuwa na mfanano usio wa kawaida wa majibu jambo ambalo si rahisi kwa wanafunzi wenye uwezo wa kufikiri tofauti.

“Jamani nawaomba wanafunzi wajitahidi kusoma kwani wakikaa kufikiri mtihani utavuja au watapewa majibu kuna hatari kubwa ya kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao au kukamatwa iwapo wataingia na majibu katika vyumba vya mitihani,” alisema Dk. Ndalichako

Aidha, alisema mwanafunzi mmoja wa Shule ya Sekondari ya Kadoto, aliandika matusi mazito katika mtihani wa Biolojia 1 kitendo ambacho ni kosa kwa mujibu wa kifungu 5 (13) cha kanuni za mitihani.

Alisema, matokeo ya watahiniwa 7,242 yamesitishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutolipa ada hasa kwa shule za serikali.

Alisema matokeo ya wanafunzi hao yatatolewa pindi mwanafunzi atakapolipa ada ya mtihani na iwapo katika kipindi cha miaka miwili wahusika watakuwa hawajalipa Baraza la Mitihani la Taifa litafuta matokeo yao.

Hata hivyo, alisema baraza hilo limetoa onyo kali kwa vituo mbalimbali vilivyobainika kufanya udanganyifu na kuvifutia usajili vituo viwili ambavyo ni Sinza Iteba na Dar es Salaam Prime kwa kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani kwa kuwa na wanafunzi wengi kuliko uwezo wake.

http://196.44.162.32/olevel.htm
http://www.necta.go.tz/html_csee209/olevel.htm