I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Wednesday, December 22

Unajua kwenye ma***nzi kuna asali, limao na shubiri?


Umeoa au umeolewa? Unataka kuolewa au kuoa? Ndiyo maswali ambayo leo ninakuuliza wewe unayeperuzi ukurasa huu. Lengo langu ni kuongea na wale wote walioamua kufunga ndoa na wale wengine ambao wako mbioni kufanya hivyo. Namaanisha waliofunga ndoa na wanaotaka kufunga ndoa, tukianza na wale ambao hawajafunga ndoa nawakata wajue kwamba ndoa si kitu cha kukifanyia majaribio kwa kukichezea kama vile ambavyo wanandoa wengi wa siku hizi wanavyofanya. Nafahamu kwamba kuna vijana na wasichana wengi ambao wanatamani kuingia kwenye ndoa huku wakiwa na imani kwamba wakifunga ndoa wataishi maisha ya raha mustarehe kama wanavyowaona wengine wanavyoishi, wenyewe wana msemo wao unaosema ‘wakubwa wanafaidi’. Kwako wewe binafsi kabla ya kuingia kwenye ndoa, unatakiwa kuwa makini na mtu ambaye unamchagua kutaka kuwa ubavu wako wa pili, unamfahamu vipi uelewa wake katika na suala zima la mapenzi. Unafahamu kwamba anayekuoa anaweza kuachana na wewe pamoja na kwamba hivi sasa mnapendana kiasi cha kufikia kuwaona watu wengine hawapendani zaidi yenu? Je, wewe na yeye mnajua kama mapenzi yamegawanyika katika ‘stage’ mbili zisizo rasmi za furaha na maumivu? Ambazo matawi yake ni asali, limao na shubiri? Ndiyo penzi linapoanza linakuwa tamu kama asali, katikati ya mapenzi chachu kama limao na mwisho na mwisho wa mapenzi huwa ni uchungu kama shubiri, je mnayajua haya? Kama mnayajua mnakabiliana nayo vipi, siku zote mimi huwa naamini kwamba penzi ni la Mwenyezi Mungu na kinyume cha penzi ni uadui ambao huletwa na shetani. Je, mnaweza kukabialiana na nguvu za shetani huyo ili ndoa mnayoota kufunga isivunjike? Kuna watu wanaichukulia ndoa kama kitu cha masihara na wala si kitu cha maana ambacho kinaweza kuwafanya kuweza kuendesha maisha yao kwa kufuata kanuni na misingi ya ndoa kama sheria zinavyosema. Nimeamua kusema hivi kwakuwa wanandoa wengi wa siku hizi hawazijui thamani ya ndoa zao walizoziingia, wengi wanachukulia kwamba unaweza kuoa au kuolewa leo na kesho ukaachana bila ya kuona haya wala kuhisi shaka. Kuna hili ambalo linahitaji uangalizi wa kina kabla ya kuingia kwenye ndoa, kwani wapo wanandoa wanaotafuta tiketi ya ndoa kwasababu zao maalumu, kama vile kufuata maslahi fulani au kuondoa mikosi kwa kuwa tu kuna mtu amejiotokeza kwa ajili ya kufunga nao ndoa. Kama hujaingia kwenye ndoa ni heri ukajiuliza mara mbili kwanini uingie kwenye ndoa? Kwanini umuoe au uolewe na huyo unayetaka ufunge naye ndoa? Hapa tunarudi kule kwenye makala yetu ya Jumatano ileee ambayo ilikuwa ikisema kwamba unamependa, anakupenda, mnapendana? Nafahamu kwamba ni vigumu kuingia kwenye ndoa kama mnaotaka kufanya hivyo hamna mapenzi ya kweli, humpendi, hakupendi na wala hampendani. Nilisema kwamba kupenda kunahitaji kujitoa kwako kwa asilimia mia kwa mia kwa mwenzako lakini kujua kama unapendwa kunahitaji ufahamu wa hali ya juu uliojaa ukamilifu wa kuweza kujiridhsisha na kukufanya uthubutu kujiingiza kwenye penzi zito. Pamoja na kwamba hakuna watu wanaopendana moja kwa moja bila ya kukwaruzana lakini mnapofikia katika hatua hiyo huwa mnakuwaje, mnayamalizaje? Hilo ndilo la msingi kabla ya kuvuka hatua kadhaa na kufikia hitimisho la kufunga ndoa. Wanawake wengi wamekuwa wakichezewa na wanaume kwa kuolewa usiku na kuachwa asubuhi na wanaume wengine wamejiamini kwamba wameoa kumbe wanajikuta wao ndiyo wameolewa na wale wanaodai kuwa wamewaoa! Unaweza kushangazwa na hili, lakini ndivyo hali halisi ilivyo katika jamii yetu kwa sasa, mwanaume unaweza kusema kwamba umeoa kumbe umeolewa, mwanamke anakuja kwako kwa lengo la kusaka mali na kisha anakuacha hoi bin taabani kwa kukufilisi kila kitu! Wangapi wamedaiwa talaka na wake zao mbele ya kadamnasi ya watu huku mke akitoa sababu zisizo na msingi na fikra zake zikiwa ni jinsi ya kugawana mali waliyoichuma, umemuoa mwanamke ambaye wala hukumjua vyema familia yake na yeye mwenyewe, mnaburuzana na kufikishana kwa Padri au Sheikh na kutaka kufunga ndoa. Huu ni uhayawani!!! Pamoja na kwamba waswahili wanasema, ukimchunguza kuku humli, lakini kabla ya kumuoa mwanamke kama huyu ulifanya utafiti wa kutosha kwamba anakupenda kweli na ulizijua tabia zake tangu awali? Mwanamke ‘kikwekwelekwe’ anaweza kukusoma udhaifu wako na kisha akakuingiza ‘kingi’ kwa kujifanya anakupenda sana kumbe anapanga kukufilisi kila kitu na kukuacha kapuku kama ‘zizi’ la kufugia kuku, upo? Siyo wanawake tu hata wanaume ‘migumegume’ iliyoshindwa na mitume nao wapo, anakuingia kwa mahaba mazito kumbe kuna kitu kwako amelenga, kwa kuwa wanawake wengi wanapenda kuolewa, basi wakijua kuwa una mali ya kutosha mwanaume anajitosa, siku mbili tatu anakutangazia ndoa. Kwa kuwa wengi wetu tunaendekeza mfumo dume, unakubali kufunga ndoa na mwanaume huyo ‘suruali’ kisha unamuandikisha mali zako, kwa kuamini kwamba mwanaume ndiye uti wa mgongo wa nyumba, basi baada ya muda yuleeee, anakutimua na anatanua na wanawake wengine kwa kutumia mali zako! Hao ndiyo wanaume na wanawake, lazima muwe makini nao katika kuingia katika ndoa zao, kwani ndoa si madoa yatakayoishia kwenye nguo, bali hufika mbali na kuangamiza raho, utakuja kuoneshwa mapenzi mazito kisha ukaachwa huna mbele wala nyuma. Naamini utakuwa na maswali kedekede, utamjuaje mlaghai, utajihami vipi? N.k ni maswali ambayo kwa hakika ni muhimu sana kwako kujiuliza, majibu yake utayapata hapa wiki ijayo katika sehemu ya mwisho ya mada hii. Utaipenda.