I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Wednesday, January 20

TAARIFA YA KIKAO CHA DHARURA CHA VIONGOZI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI WA KITANZANIA HYDERABAD INDIA (TSAH)

viongozi wa jumuiya ya tsah mwenye shati la mistari rangi nyeupe ni M/KITI ABDILLAH NKYA, NA SHATI JEKUNDU MAKAMU M/KITI SHAH,MWENYE SHATI NYEUPE KATIBU MKUU,KULIA KWA MAKAMU NI KATIBU MWENEZI,ALIEVAA MIWANI MUWEKA HAZINA NA KUSHOTO KWA MAKAMU NI MJUMBE WA KAMATI YA KATIBA BWANA AGNEULUS KAYOMBO

































Ndugu Watanzania pamoja na Wanajumuiya ya wanafunzi Hyderabad nchini India.

Kama mnavyojua, hali ya kisiasa katika Jimbo la Andhra Pradesh si shwari kutokana na vurugu za kisiasa za kuishinikiza Serikali ya India itenge Jimbo huru la Telangana. Vurugu hizi zimetawala zaidi katika vyuo Vikuu hususan Osmania (Osmania University) ambacho watanzania walio wengi wanasoma katika Chuo hiki.

Kufuatia hali hiyo, Mitihani ya Semister imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara tangu Mwezi November, 2009. Takribani miezi miwili na nusu sasa. Aidha kumekuwa na migomo ya wanafunzi (wahindi) kuingia madarasani hadi hapo Jimbo hilo litakapotengwa. Hali hii imetuathiri kwa kiasi kikubwa kisaikolojia ambapo hadi sasa haijulikani mitihani hiyo itafanyika lini na lini hasa wanafunzi (wahindi) watakapokubali kuingia madarasani na kukubali kufanya mitihani. Kutokana na hali hii upo wasi wasi mkubwa wa kufutwa kwa Mwaka wa masomo kama inavyoelezwa na uongozi wa Chuo.

Ni wazi ifahamike kuwa vurugu hizi ni za kisiasa na hazihusishi mwanafunzi yeyote wa kigeni (Foreign students) isipokuwa wanafundi wakihindi wanaoshabikia siasa. Hata hivyo athari za kutofanyika mitihani kwa wakati napengine kufutwa kwa mwaka wa masomo zinatuathiri wote kwa pamoja kama vile kupoteza muda mwingi bila kuingia madarasani, kusoma na kufanya mitihani. Mbaya zaidi tunaweza kupoteza mwaka wa masomo kama dalili zinavyojionyesha.

Ndugu wanajumuiya, kuahirishwa kwa mitihani ni upotevu wa muda na ikitokea kufutwa kwa mwaka wa masomo ni usumbufu kwetu na upotevu wa gharama.

Kutokana na hali hiyo, leo tarehe 20.01.2010 Uongozi wa Jumuiya umefanya kikao cha dharura kujadili suala hili na kuamua kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuandika barua maalum kwa Uongozi wa Chuo ili utoe msimamo wake juu ya hatima ya wanafunzi wakitanzania wanaokumbwa na athari za vurugu hizi. Pia kikao kimeazimia kulifikisha rasmi (kwa barua) suala hili katika Ubalozi wetu New Delhi.

Mwenyekiti wa Jumuiya anawaomba watanzania wote kuwa wavumilivu wakati huu ambao suala hili linafuatiliwa na kufanyiwa kazi. Waendelee kujisomea majumbani na kujianda na mitihani muda wowote itakapoamriwa. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

ABDILLAH DAUD NKYA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania Hyderabad - India