I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Sunday, January 24

OSAMA BIN LADEN KUHUSIKA NA JARIBIO LA KUILIPUA NDEGE YA MAREKANI
Kiongozi wa Al-Qaeda Osama bin Laden ametoa kanda mpya ya sauti, akidai kubeba dhamana ya kuhusika na jaribio ambalo halikufaulu la kuiripua ndege ya shirika la ndege la Ki-Marekani siku ya Krismasi.

Katika taarifa hiyo iliyoonyeshwa kupitia televisheni ya Al-Jazeera, Bin Laden alimtumia ujumbe rais Barack Obama akisema mashambulizi dhidi ya Marekani bado yataendelea, na kwamba Marekani haitokuwa na amani hadi pale Wapalestina watakapopata amani.

Kijana wa Ki-Nigeria Umar Farouk Abdul Mutallab ameshafunguliwa mashtaka ya kujaribu kuiripua ndege hiyo ya shirika la ndege la Delta Airlines, ilipokuwa inawasili katika uwanja wa ndege wa Detroit, kutoka mjini Amsterdam. Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 300.