Mshambuliaji wa timu ya Bongo Freva,Ali Kiba akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya Bongo Movie katika mtanange wa Kuchangia maafa ya Gongo La Mboto uliomalizika jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Bongo Freva iliibuka kidedea kwa mabao 2-0 yaliyotiwa kimyani na mshambuliaji H. Baba katika kipindi cha kwanza cha mchezo.
Kiungo wa Bongo Movie,Ben Kinyaiya akipiga penati na kuipaiza juu ya mashabiki....
Mshambuliaji wa kushoto wa timu ya Bongo Freva,KR Mullah akimtoka mchezaji wa timu ya Bongo Movie katika mchezo uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa.
Mshambuliaji wa timu ya Bongo Freva,H. Baba akiipachia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Bongo Movie katika mtanange wa kuchangia maafa ya Gongo la Mboto uliopigwa jioni hii katika uwanja wa Taifa jijini Dar.
Hatari langoni mwa Bongo Movie.
Nyanda wa timu ya Bongo Fleva,Tunda Man akionyesha utaalamu wake mbele ya mchezaji wa timu ya Bongo Movie,Joti katika mtanange uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar.Hapa Joti ulimi ng'ombe
Bongo Fleva wakishangilia ushindi waoo.
Vingwanga vilitawala kabla ya mchezo kuanza kwa upande wa wana Bongo Movie.
Mgeni Rasmi katika mchezo huo,Meya wa Ilala,Mh. Jerry Slaa akikagua timu kabla ya mchezo.
Timu ya Bongo Movie.
Timu ya Bongo Freva.
Uwanja ulifurika sana kwa kweli,hii inaonyesha ni kiasi gani watu walivyohamasika katika swala zima la kuchangia wahanga wa mabomu kule Gongo la Mboto.
Hawa ndio wazoefu wa kitaa hicho cha tolichowki udocni,wa kwanza kulia kwako ni Mkiti mstahafu wa jumuiya ya wanafunzi waishio hyderabad Bw.Abdillah Nkya akifatiwa na Mr.Nassib ,Mr said aka Dr Matata ambaye hajawahi kukaukiwa na stori za maskani hata siku moja akifuatiwa na Bw.Alex,Bw.Habib maarufu bwana kudo nyuma ya aliyevaa shati namba 10,mwenye nyekundu bwana Ally na mwenye jezi no 10 ni.Mr Hashim
Mr Nkya na bw. Mohammed maarufu urary 95
kikosi kizima cha tolichowki ...kusema ukweli ule msemo wa ''umoja nguvu na mshikamano''unapatikana kwenye hii picha
huwezi kuamini hawa watanzania walivyokuwa na umoja na mshikamano....umoja huu walijengea na nchi yao hivyo wanaudumisha hata wakiwa kwenye nchi za watu
Hapa kuna kichwa cha computa ,sheria ,hesabu na habari gusa unase....
''nipe gwala.....................''
wakongwe wa tolichowki india wako zaidi ya miaka 3...
Hapa Bw Tabagi akigawa t shirt zenye kuonesha utamaduni wa kitanzania..
''Huyu dogo anapenda sana kutafuna kijiti....''
Hapa anatafuta kijiti kingine......
Miss Dina akijaribu T shirt yenye kuonesha utamaduni wa kitanzania kutoka kwa Bw Tabagi
Bw.Tabagi akionesha T.shirt zinaonesha utamaduni wa kitanzania ...
Huyu ni Mr.Adam na Mr Patrick..... wakionesha ushirikiano waliokuwa nao..Hapo kuna kichwa cha uchumi na computa
Mr Nassib huyu ni kichwa kwenye masuala ya network na makorokoro yote ya Java..
Hapa ni mpango mzima wa kupeleka pwani....shiba upate mwili
''Eti tabagi hiyo Tshirt bei gani..?,......rupees 400/=tu....
Miss Dina nae hakuwa nyuma ..ni ktk mamis wanaojitolea kuendesha libenenge la umoja wa wanafunzi waishio hapa mjini hyderabad india
kulia kwako wa kwanza ni Mr.Joseph Makwinya huyu ndie aliyeandaa shughuli hii ...ambapo pamoja na kubadilishana mawazo ya hapa na pale ..alihakikisha kila mtu anagonga mishkaki kadhaa,kuku wakuchoma ,kinywaji cha kulainisha koo,na hata kwa wale wapenzi wa viepe pia alihakikisha nao wanavisinabuda
kwa kweli inafurahisha sana wanafunzi wakigeni tunapokutana kama hivi ,na kujadili mambo mbalimbali,ya kwetu na nyumbani Tanzania yaani unasikia furaha 90 degree angle
Leo ni siku ya kuzaliwa Miss Ishya Dallo 25.feb,blog hii na kwa niaba ya ndugu zake wa karibu tolichowki,Malakpet na sainikpuri Hyderabad,wote kwa pamoja tunamtakia furaha yeye na familia yake yote M/Mungu ampe afya njema ktk maisha yke na mafanikio ktk siku zake nyingine za usoni karibu sana dada yetu we wish u happy Bday
Leo ni siku ya kuzaliwa Mkiti mstahafu TSAH Mr Abdillah D.Nkya 22.feb,blog hii na kwa niaba ya ndugu zake wa karibu tolichowki na sainikpuri Hyderabad,wote kwa pamoja tunamtakia furaha yeye na familia yke yote M/Mungu ampe afya njema ktk maisha yke na mafanikio ktk siku zake nyingine za usoni karibu sana kwenye huu ulimwengu wa samaki wakubwa wanaoishi kwa kutegemea samaki wadogo...utaupenda tu...
Marehemu Nickson Membi Jumuiya ya wanafunzi wa kigeni mjini hyderabad India (TSAH) inasikitika kutangaza kifo cha mwanafunzi mwenzao Nickson Membi kilichotokea leo alfajiri tar 13 feb.2011 maeneo ya singapore city hyderabad kwa ajali ya gari,Jumuiya ya TSAH inawaomba wanafunzi wote na ndugu na jamaa kufika kufika nyumbani kwa M/kiti kwa wamwanzamwanza sainikpuri ambapo taarifa zaidi zitatolewa kwani mwili wa marehemu unategemewa kusafirishwa kuelekea Tanzania Tulikupenda sana lakini M/mungu amekupenda zaidi
Leo ni siku ya kuzaliwa Dr.Abdul aziz Ally 12.feb,blog hii na kwa niaba ya ndugu zake wa karibu tolichowki na sainikpuri Hyderabad,wote kwa pamoja tunamtakia furaha yeye na familia yke yote M/Mungu ampe afya njema ktk maisha yke na mafanikio ktk siku zake nyingine za usoni karibu Dr, kwenye huu ulimwengu wa papa na nyangumi utaupenda tu una kila sifa utakazo zihitaji...
WABUNGE wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe jana walichafua hali ya hewa bungeni pale walipotoka tena nje ya Ukumbi ya Bunge kupinga azimio la kuondoa utata wa tafsiri ya Kanuni ya Bunge inayotoa fursa kwa chama chenye asilimia 12.5 ya wabunge wote kuunda kambi rasmi ya upinzani.
Tukio hilo linalofanana na lile la Novemba 18, mwaka jana, Rais Kikwete alipozindua Bunge lilifanywa na Chadema baada ya Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro kuchangia mjadala wa huo akiwa mchangiaji wa mwisho.
"Madamu Bunge limeona busara kuleta hoja hii, na vijembe vile, kwa masikitiko nasema hatutashiriki kumalizia hoja hii, naomba kutoa hoja," alimalizia maelezo yake Mbowe na kuanza kutoka nje akifuatiwa na wabunge wa chama hicho.
Hata hivyo, wakati wabunge hao wa Chadema wakitoka nje, wabunge waliobaki wengi wakiwa wa chama tawala CCM, walisikika wakitoa maneno ya kebehi dhidi ya wabunge wa Chadema.
"Tumewazoea kukimbia, kwisha, uchoyo, weak politicians, na kwenye posho msije, mnadaiwa na mabenki,"walisikika wabunge wakisema kwa kupiga kelele.
Awali Mbowe akichangia mjadala huo alisema kuwa ushirika ni jambo la msingi, lakini katika Bunge la Kumi kuna tofauti za msingi.
"Bunge la Kumi kuna tofauti za msingi, haki ya kila chama haiondolewi kwa dhana za juu juu. Kuchagua mshirika ni haki yetu kikatiba na hatuwezi kulazimishwa ndoa, tumeona vijembe vilivyotokea leo tutawezaje kuwa na kambi moja?. Tunahitaji muda zaidi" alisema Mbowe na kuongeza:
“Ni vigumu ukalazimishwa uchumba na mtu hivyo hivyo hatuwezi kulazimishwa katika ushirikiano,’’ alisema na kuongeza: “ Hakuna trust(uaminifu) katika ushirika huu.’’
Aliongeza: "Viongozi wa vyama kushirikiana ni vizuri, tupeane muda, maridhiano hayawezi kuwa ndani ya wiki moja au mbili. Uamuzi wenu unabomoa, kwani hapa tatizo si tafsiri bali dhana ya ushirika tunaotaka bungeni. Yapo ya msingi, lakini si kutulazimisha kuingia katika jambo ambalo hatujaridhia."
Mbowe alisema tofauti zilizopo zinazungumzika huku akionya kuwa wingi usitumiwe kugandamiza Chadema na kwamba kanuni zisitumiwe kuua msingi wa haki ambapo pia alieleza kuwa chama chake hakitakubali hilo na ndiyo dhamira ya Chadema.
Wakati wakitoka kwenye ukumbi huo, majira ya saa 11:30 jioni wabunge wengine wa CCM, TLP, NCCR-Mageuzi, UDP na CUF walioonekana kushikwa butwaa kwa kitendo hicho.
Mkutano na Waandishi wa Habari
Baada ya kutoka nje, Mbowe alizungumza na wanahabari, mkutano ambao ulirushwa moja kwa moja na Kituo cha Televisheni cha Star (Star TV).
Katika mkutano huo, Mbowe alisema wataendelea kupinga vitendo vyote vinavyovunja Kanuni za Bunge kwa maslahi ya Bunge na Taifa.
"Hatutawaheshimu kamwe wabunge 'wanaocompromise' haki zao (wanaokubali haki zao kudhulumiwa), na tutaendelea kupinga kilichotokea leo, ndani na nje ya Bunge," alisema Mbowe. Hata hivyo, baada ya kumalizika na kupitishwa marekebisho hayo ya kile kilichoelezwa kuwa kuondoa utata wa tafsiri katika kanuni ya 14 hadi 16 ya Bunge, wabunge hao wa Chadema walirudi ndani ya Ukumbi wa Bunge na kuzua tena maneno ya chini chini kutoka kwa wabunge.
Kwa kupitishwa mabadiliko hayo na kwa mujibu wa kanuni ya 15(2) tafsiri ya Kambi Rasmi ya upinzani bungeni ni kambi inayoundwa na vyama vya upinzani vinavyowakilishwa bungeni.
Hata hivyo, bado Chadema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge ndicho kitakachotoa Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni na naibu wake. Pia kiongozi huyo ana mamlaka na uhuru wa kuteua Baraza la Mawaziri Kivuli kutokana na wabunge wa upinzani waliopo.
Hata hivyo, azimio hilo linaondoa dhana iliyokuwepo kwamba Chadema ndicho kingetoa wenyeviti wa Kamati za Hesabu za Serikali ambazo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge zinatakiwa kuongozwa na wapinzani.
Tofauti na ilivyokuwa ikifahamika awali, mabadiliko ya jana yanatoa fursa kwa mbunge yeyote wa upinzani kugombea nafasi hizo bila kuhitaji idhini ya uongozi wa kambi ya upinzani.
Wachunguzi wa mambo ya siasa wanaiona hatua hiyo kuwa ni kuwanyima Chadema nafasi ya kuongoza kamati hizo, kwani kwa kuzingatia uhusiano wake mbaya na CCM ni dhahiri nafasi za wenyeviti zitakwenda kwa vyama vya CUF, NCCR – Mageuzi , TLP au UDP ambavyo wabunge wake walikuwa wakiunga mkono azimio la kuingizwa kwa tafsiri hiyo katika Kanuni za Bunge.
Spika Anne Makinda Kabla ya kuhitimishwa kwa hoja hiyo iliyopigiwa kura na kupitishwa, Spika wa Bunge, Anne Makinda alisema kuwa: "Katika hoja hii, Chadema haikuwa na ukweli, wananchi wajue hili. Wenzetu wamepitiwa. Kitendo kilichotokea hapa si utaratibu mzuri, watawaambia nini wananchi?."
Spika alionekana kukerwa na kitendo hicho cha Chadema na kuhoji iwapo kweli wabunge hao wapo kwa ajili ya maslahi ya umma au maslahi yao wenyewe.
Hata hivyo, mkutano wa Bunge uliendelea kwa Naibu Spika, Job Ndugai kufafanua baadhi ya vipengele vinavyohalalisha uwepo wa kambi ya upinzani bungeni.
Kwa pamoja wabunge waliobaki walipitisha azimio la kuwepo kwa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Vijembe vya Mrema na Lusinde Mbunge wa Jimbo la Vunjo(TLP), Augustine Mrema pamoja na Livingstone Lusinde wa Jimbo la Mtera (CCM) waliwapiga vijembe Chadema wakati wakichangia hotuba ya Rais Kikwete aliyoitoa Novemba 18 mwaka jana alipokuwa akizindua rasmi Bunge la Kumi.
Mrema aliwapiga vijembe Chadema akisema alistahili kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kutokana na uzoefu pamoja na sifa alizonazo.
“Nimekuwa mbunge mara tatu kwa vyama vitatu tofauti, nimekuwa naibu waziri mkuu, nikakamata kontena la dhahabu, niliweza kupambana na ufisadi hivyo nilistahili kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani,” alisema Mrema.
Naye Lusinde alikwenda mbali na kusema kutokana na viongozi kuonekana kuchoshwa na amani iliyopo, alipendekeza wabunge wapigane bungeni ili wajue uchungu wa kupoteza amani.
“Nafikiri kuliko kuwashawishi kwanza wananchi wavunje amani kwanza ningependa kuona siku moja bungeni humu wabunge tukizichapa ili tujue uchungu wa kupoteza na si tu kuwashawishi wananchi halafu sisi viongozi hatudhuriki na tunajipatia sifa za bure,’’ alisema Lusinde
Sugu nakubalika kila mahali...'dogo itamuuma sna...lkn ndio maisha this is power... Jaffarai *****shy rose
nimeachana na shyrose bhanji (kicheche mzee)baada ya kugundua km anatoka kimapenzi na mr 2... ni aibu sana kwa mwanamke mwenye miaka 42 kua kicheche kiac hicho!!!! nilitegemea mtu km mr 2 angeanza kufanya harakati ktk mziki wetu lkn harakati zake zimehamia kwenya mapenzi na madem wa wasanii wenzake... ni aibu kubwa sana