I WISH U A MARRY XMASS & HAPPY NEW YEAR 2012

click the word video above 2 watch the clips & cloz 2 back

Saturday, January 29

Cheka...urefuke..


Friday, January 28

Sijaona cha kukupa duniani...labda Mungu kakuandalia zawadi mbinguni

''unajua kuvumilia... uko juu nakwambia...kwenye huu mchezo unamudu c mchezo..sifa zimuendee kungwi wako''

Thursday, January 27

Huyu binti ndie aliyeongoza matokeo ya kidato cha nne 2010 jinchi lote la TZ..Nimeipenda pics yke,ur welcome!!!

Lucy mallya
*Nusu ya wanafunzi waambulia daraja 0
*Wasichana hawashikiki, wavulana hoi
*Katika kumi bora wachukua nafasi nane
*Shule za Dar, K`njaro, Moro, Mbeya juu
Matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyotangazwa jana yanaonyesha kwamba wasichana wamewapiku kwa mbali wavulana, wakikalia nafasi nane kati ya kumi bora, huku nusu ya watahiniwa wote wakiambulia daraja sifuri.

Katika matokeo ya mtihani huo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako, jumla ya watahiniwa 352,840 waliofanya mtihani huo ni 177,021 tu waliofaulu.

Matokeo ya mtihani huo uliofanyika mwaka Oktoba mwaka jana pia yanaonyesha kuwa watahiniwa wanne wamefutiwa matokeo kwa kuandika matusi mazito kwenye karatasi za kujaza majibu.

Matokeo hayo yanaonyesha kuwa shule binafsi 10 ndizo zinazoongoza katika kundi la shule kumi bora kitaifa zilizofanya vizuri.

Dk. Ndalichako alisema watahiniwa wa shule waliosajiliwa ni 363,589, lakini waliofanya mitihani ni 352,840, waliofaulu wakiwa ni 177,021 sawa na asilimia 50.4.

Katika kundi la waliofaulu, wasichana ni 69,996 sawa na asilimia 43.3 na wavulana ni 107,025 sawa na asilimia 56.

Alisema watahiniwa binafsi waliosajiliwa walikuwa 94,525 na kati ya hao waliofaulu walikuwa 46,064 sawa na asilimia 52.

Katika ubora wa ufaulu kwa kuangalia madaraja waliyopata watahiniwa wa shule, Dk. Ndalichako alisema 40, 388 sawa na asilimia 11.5 wamefaulu katika madaraja ya I hadi III na kwamba wasichana waliofaulu katika madaraja hayo ni 12,583 na wavulana ni 27,805.
Alisema jumla ya wanafunzi waliopata daraja 0 ni 174,193 ambao ni karibu nusu ya wanafunzi wote waliofanya mitihani hiyo.

Jedwali la matokeo linaonyesha kuwa wavulana waliopata darala la kwanza I ni 3,874 na wasichana ni 1,489, daraja la II wavulana ni 7,003 na wasichana ni 2,939, daraja la III wavulana ni 16,928, wasichana ni 8,155 na daraja la IV wavulana ni 79,220 na wasichana ni 57,413.

SHULE KALI 10

Alitaja shule 10 zilizoongoza kitaifa na mikoa yake katika mabano kuwa ni Uru Seminary (Kilimanjaro), Marian Girls (Pwani), St Francis Girls (Mbeya), Canossa (Dar es Salaam), Msolwa (Morogoro), Feza Boys (Dar es Salaam), St Mary Goreti (Kilimanjaro), Abbey (Mtwara), St Joseph’s Sem Iterarambogo (Kigoma) na Barbro-Johanson (Dar es Salaam).

WANAFUNZI WAKALI 10

Aliwataja wanafunzi bora 10 kitaifa ambao walifanya vizuri kuliko wote na shule zao katika mabano kuwa ni Lucylight Mallya na Maria-Dorin Shayo (Marian Girls).

Wengine ni Sherryen Cessar (Barbro-Johanson), Diana Abel Matabwa (St Francis Girls), Neema Joey Kafwimi (St Francis) na Beatrice Issara (St Mary Goreti).

Wengine ni Johnston Dedani (Ilboru) mkoani Arusha, Samwel M. Emmanuel (Moshi Tech), Bertha Sanga (Marian Girls) na Bernadetha Kalluvya (St Francis Girls).

Aliwataja wavulana kumi walioongoza kitaifa kuwa ni Johnston Dedani (Ilboru), Samwel Emmanuel (Moshi Tech), Jimoku Salum (Shinyanga Sekondari), Amaniel Barabara (Arusha Day), Aswile Mwambembe (Kibaha), James Mwitondi (Loyola), Gasper Mung’ong’o (Loyola), Yohane Kihaga (Don Bosco Seminary (Iringa) na Tonny Tarimo wa (Msolwa, Morogoro).

Dk. Ndalichako alisema Necta inashikilia matokeo ya watahiniwa 1,448 waliofanya mitihani bila kulipa ada hadi hapo watakapolipa pamoja na faini katika kipindi cha miaka miwili.

Alisema watahiniwa 311 wamefutiwa matokeo yao baada ya kubainika kuwa walifanya udanganyifu wa aina mbalimbali.

Katika hatua nyingine, Dk. Ndalichako aliwaonya wanafunzi wa kidato cha sita ambao wanatarajia kufanya mitihani yao mwezi ujao kuacha kuandika matusi kwenye mitihani yao hata kama imewashinda.

“Nawaomba kidato cha sita wasifanya mchezo huu kabisa, maana inaonekana kama inaanza kuwa mazoea. Mwaka jana kulikuwa na mwanafunzi mmoja aliyeandika matusi kwenye karatasi ya majibu mwaka huu idadi imeongezeka na kuwa wanne,” alisema Dk. Ndalichako.
nibofye kusoma matokeo haya...
http://www.necta.go.tz/matokeo2010/csee2010/olevel.htm

Tuesday, January 25

Bahari ambayo mtu hawezi kuzama

shemeji akielea juu ya maji ya dead sea
SI rahisi kuamini kwamba kuna bahari au ziwa lolote duniani ambapo mtu akiingia hawezi kuzama. Lakini, kwa waliowahi kufika Mashariki ya Kati na kuiona bahari inayojulikana kama Dead Sea,

wakajaribu kuingia katika maji yake au kuwaona watu waliokuwa wakielea katika maji hayo huku wakisoma magazeti, wanaamini tangu siku hiyo.

Inaitwa Dead Sea ambapo tafsiri yake kwa Kiswahili ni “Bahari Iliyokufa”. Iliitwa hivyo kutokana na ukweli kwamba maji yake yana chumvi nyingi mno kiasi kwamba si rahisi kwa viumbe vyenye uhai kuishi katika maji yake.

Kwa Kiarabu, bahari hiyo inaitwa “al-Bahr al-Mayyit” na kwa Kiyahudi inaitwa “Yam Ha-Mela” yote yakimaanisha “Bahari ya Chumvi”.

Ifahamike pia kwamba pamoja na eneo hilo la maji kuitwa bahari, kwa kweli ukubwa wake ni kama ziwa la kawaida tu.

Bahari hiyo ambayo pia huitwa Salt Lake yaani “Bahari ya Chumvi”, iko katikati ya Jordan kwa upande wa Mashariki.Upande wa Magharibi inapakana na Israel na Ukingo wa Magharibi (Palestina).

Uso wake na kingo zake ziko mita 422 chini ya usawa wa bahari, ambacho ni kipimo cha chini zaidi katika uso wa dunia katika eneo lililoko katikati ya ardhi kavu.

Ikiwa moja ya bahari au maziwa yenye chumvi nyingi zaidi, Dead Sea maji yake yana chumvi kwa asilimia 33.7, japokuwa maziwa Assal lililoko Djibouti na maziwa ya McMurdo Dry Valleys eneo la Antarctica (kama vile Don Juan Pond) yana viwango vya juu zaidi vya chumvi.

Dead Sea ina kiwango cha chumvi ambacho ni mara 8.6 zaidi ya kile kilichomo katika bahari. Hivyo, wingi huo wa chumvi ni moja kwa moja hauwezi tena kuruhusu viumbe hai kuishi ndani yake, na ndiyo maana ikaitwa Bahari Iliyokufa.
Hata hivyo, kuna aina fulani za bakteria na mimea ambayo huweza kuishi katika maji hayo. Kwa kifupi, mazingira ya Dead Sea yako sawa kabisa na ziwa liitwalo Great Salt Lake lililoko Utah, nchini Marekani.

Urefu wa ziwa hilo ni kilomita 67 na upana wake (katika sehemu ndefu zaidi) ni kilomita 18, na mto pekee unaomwaga maji ndani yake ni Mto Jordan.

Uzito wa maji yake ni kilo 1.24, jambo ambalo linafanya uogeleaji ndani yake kuwa mgumu, lakini maji hayohayo hutoa burudani tosha. Mtu unaweza ukajilaza juu yake ukabaki unaelea muda wote huku ukisoma gazeti au ukinywa bia!

Maajabu ya bahari au ziwa hilo, ambalo katika Biblia, linatajwa liliwahi kuwa makimbilio ya Mfalme Daud (David) ni kwamba imekuwa ikivutia maelfu ya watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Ilikuwa pia ni moja ya vituo vya mwanzo duniani vya tiba tangu enzi za mfalme “Herod the Great”.

Miongoni mwa bidhaa zinazopatikana katika bahari hiyo ni chumvi za aina ya “potash”, mbolea, madawa ya kuhifadhia viumbe visioze, na kadhalika.

Nadharia zilizopo ni kwamba kiasi cha miaka milioni tatu iliyopita kile ambacho leo ni bonde la Mto Jordan, Dead Sea na Wadi Arabah lilikuwa kila mara linafurika maji kutoka Bahari ya Mediterranean. Maji yaliyokuwa yakifika huko kutokea kupitia Bonde la Jezreel.

Mafuriko hayo yalikuwa yakilikumba eneo hilo na kutoweka kufuatana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Matokeo yake ni kwamba ziwa ambalo lilikuwa katika eneo la Dead Sea, ambalo liliitwa “Ziwa Sodoma”, lilibakia na marundo ya chumvi ambayo unene wake ukafikia kilomita tatu.

Hivyo, baada ya mafuriko hayo kukoma, eneo hilo likabaki na maji na chumvi katika kile kinachojulikana leo kama Dead Sea.
Kama ilivyotajwa mwanzoni, bahari hiyo imekuwa ni kituo kikubwa cha tiba kwa magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na magonjwa ya ngozi ambapo walioathirika huoga maji yake,

wakaishi kwa muda sehemu hiyo ambayo iko chini ya usawa wa bahari, jambo ambalo hupunguza ukali wa mionzi ya madhara ijulikanayo kama “ultraviolet”.

Sunday, January 23

Noti mpya tz zamwaga rangi ..angalia usivae na suti nyeupe au kuiweka mdomoni ..

Sadick Mtulya

UBORA wa noti mpya zilizoanza kutumika mwanzoni mwa mwaka huu unatia shaka, baada ya kubainika kuwa baadhi yake zinachuja na kuacha rangi zikilowa maji au jasho.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi Jumapili umebaini kuwa noti hizo hasa za Sh5,000 na Sh10,000 zikikandamizwa au kusuguliwa kwenye karatasi nyeupe hata bila kuloweshwa maji au jasho, huacha rangi. Hali hii imesababisha baadhi ya watu kuanza kutilia shaka ubora wake huku wasomi wakitaka serikali kuwa makini kwa

Lawrence Mkina ambaye Mkazi wa jijini Dar es Salaam aliliambia gazeti hili kwa njia ya simu jana kuwa haamini kama noti mpya kama zina ubora unatakiwa. Alisema aliweka kwenye mfuko wa shti lake jeupe noti za sh 5,000, lakini baadaye alipozitoa shati lilikuwa limechafuka kwa rangi ya noti.

Mkina alisema huenda noti hizo zimechachakuliwa na wanjanja mitaani kwani hata ukiisugua katika karatasi nyeupe zitacha rangi kama ‘carbon paper’. Ili kuthibitisha malalamiko hayo, Mwananchi Jumapili ilichukua noti mpya ya sh 5,000 na kuisugua kwenye karatasi ya nyeupe ikaacha rangi ya bluu.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Dk Honest Ngowi alieleza madhara ya noti zisizokuwa na ubora kuwa ni pamoja na kugushiwa kirahisi.

“Ubora wa noti ni kitu muhimu na kama ikikosa ubora inaleta maswali mengi na moja ya athari itakayojitokeza ni kugushiwa kirahisi,’’ alisema Dk Ngowi. Dk Ngowi ambaye ni mwanazuoni aliyebobea katika taaluma ya uchumi, alisema noti ikikosa ubora, huchakaa mapema na kuleta utata katika kukubalika kwenye soko. “Kutokana na kuchakaa mapema, serikali italazimika kuchapisha noti nyingini hali ambayo italigharimu taifa fedha nyingi katika muda mfupi. Pia inawezekana nchi za Jumuiya ya Afrika ya Afrika Mashariki, zikakataa kuzitumia noti hizo,’’ alisema.

Kuhusu sifa na ubora wa noti, Dk Ngowi alisema ni lazima iwe katika kiwango bora ikiwamo kuwa na karatasi ngumu isiyochakaa na kuchanika mapema na kuwa na uzito. Akizungumzia suala hilo, Gavana wa Benki Kuu, Profesa Benno Ndullu alisema BoT inafuatilia matatizo yanayojitokeza katika noti hizo mpya kwa karibu na kuyafanyia kazi.

“Hili linawezekana ingawa wewe ndio mtu wa kwanza kujitokeza kueleza, lakini kama tatizo hili lipo, tutalifanyia kazi,’’ alisema Profesa Ndullu. Akaongeza: “Kwa sasa BoT ina-monitor (inafuatailia) kwa ukaribu usambazaji wa noti mpya pamoja na kuangalia matatizo yanayojitokeza na kuyafanyia kazi haraka iwezekanavyo.’’ Gavana huyo alisema matatizo yote yatakayojitokeza katika noti hizo yatafikishwa kwa mzabuni aliyezichapisha ili kufanyiwa kazi. Kabla ya kuchapishwa noti hizi, Benki Kuu iliahidi kuwa noti mpya zitakuwa imara ambazo hazitaweza kugushiwa kirahisi.

Tatizo la noti hizo mpya limejulikana siku nne baada ya watu watatu kukamatwa Januari 20, mwaka huu, mkoani Ruvuma wakitengeneza noti za bandia kwenye nyumba ya kulala wageni. Kamanda wa Polisi mkoani humo, Michael Kamuhanda, alisema watu hao ambao wote ni wakazi wa eneo la Bombambili, walikamatwa saa tano usiku katika nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa Matomondo, eneo la Misufini. Alisema siku ya tukio, polisi wakiwa kwenye doria waliwakamata watuhumiwa hao wakiwa na karatasi zinazodaiwa kutumika kutengenezea noti bandia.

Saturday, January 22

lets be quite...
Tuesday, January 18

Ona kokwa upande wa ndani...

hebu ona huyu ****alivyochojoa...

Monday, January 17

Is katrina kaif the princess of popcorn?


Katrina has left home most of her clothes and is pompously flaunting her belly button in this song whose lyrics are as provocative as is its video. In fact, such a hysteria has spawned over the song that google engine is working overtime to meet the demands of the male voyeurs and Katrina die-hards.

.While no one is quite complaining but it’s a matter of great speculation if Katrina’s belly show highlights her sexiness or is it ill-suitable to an actress of her stature. After all, the blatant show of navel is still a taboo subject in many Indian corners and some quarters may consider it objectionable and obnoxious.

But then, going by the modern demand of the industry, the westernisation of the youths and the liberalisation of mainstream cinema, Katrina’s bold skin show is only going to earn her some brownie points and cement her position as the princess of popcorn. What’s your opinion?

Sunday, January 16

Saturday, January 15

Ajifungua mkono mzima ....madaktari hoi...


Bi.Shija Maige (33)mkazi wa Kahama Mkoani Shinyanga amejifungua watoto 5.Yeye na watoto wake 5 wana afya ile mbaya.

Thursday, January 13

Snoop dogg -wet

Kanye West Buys $180k Watch of Himself!


THIS IS SOME CRAZY WATCH THAT KANYE WEST JUST PURCHASED FOR $180K! WHAT DO YOU THINK?

Usilie kwa ajili ya mapenzi mpira ni dakika 90....


NI wiki nyingine tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba kwa rehema zake Mwenyezi Mungu umzima na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku kama kawaida. Mimi nashukuru naendelea vizuri na majukumu yangu likiwemo hili la kukuandikia mada ambazo kwa namna moja ama nyingine zinagusa maisha yako ya kila siku hasa linapokuja suala la mapenzi. Wiki hii nataka kuzungumza na wale ambao mapenzi yamekuwa yakiwafanya wakose raha kabisa katika maisha yao na kufikia hatua ya kukufuru kwa kutamka maneno yasiyofaa. “Jamani nimemkosea nini Mungu mimi? Yaani nimekuwa mtu wa kulizwa kila siku kwa sababu ya mapenzi. Mbona rafiki zangu wametawaliwa na furaha katika maisha yao, mimi nina kasoro gani?” Haya ni maneno ambayo unaweza kuyasikia kutoka kwa msichana au mvulana ambaye ameona mapenzi hayamtendei haki. Lakini sasa kuna jambo nataka kulisema kwa wale ambao wako katika hali hiyo. Kwanza, tufahamu mapenzi yanaua! Hilo halina ubishi. Wapo waliojikuta wanaumwa vidonda vya tumbo na mwishowe kufariki dunia kwa sababu ya mapenzi. Wapo waliodiriki kujiua kwa sababu wamekataliwa au wametendwa na watu waliotokea kuwapenda kupitiliza. Kwa kifupi, mapenzi ni kitu ambacho kila mmoja anatakiwa kuwa makini nacho kwa kuhakikisha hakiyaathiri maisha yao ya kila siku. Tunatambua kwamba kila mmoja ana moyo wa kupenda lakini sasa tunatakiwa kuangalia mahali pa kupenda. Siyo kila wakati tuuachie moyo ufanye maamuzi, wakati mwingine moyo wako unaweza kukuingiza kwenye matatizo kwa kujikuta unapenda pasipo na penzi, mwishowe ukawa ni mtu wa kuumizwa kila siku. Labda tuangalie mambo yanayowafanya baadhi ya watu kuwa ni wa kutoa machozi kila siku. Kwanza kulia kutakuwa hakuepukiki kwa mtu yoyote endapo atakubali kuangukia kwa mtu asiye na mapenzi naye. Hivi furaha itatoka wapi kama kweli mtu uliyemkabidhi moyo wako atakuwa hajakupa nafasi katika moyo wake? Ni wazi utalia kwani kusalitiwa itakuwa ni jambo lisiloepukika, kupuuzwa, kutothaminiwa pamoja na kutooneshwa mapenzi ya dhati. Pia unaweza kutokea kumpenda mtu flani ambaye naye anakupenda lakini hajatulia. Watu wa aina hii wapo huko mtaani. Yaani anakupenda wewe lakini bado haridhiki na kile anachokipata kutoka kwako. Matokeo yake naye anakuwa mwepesi wa kukusaliti na hata pale unapokuja kugundua, hujuta sana na kuomba msamaha kwa kulia kuonesha kuwa, alichokifanya hakitokani na kutokukupenda, bali ni tamaa zake. Ndiyo maana mara kwa mara nimekuwa nikisema, mapenzi ni sawa na kucheza kamari. Nikimaanisha kwamba, unapotokea kumpenda mtu utarajie mawili, aidha na yeye kuwa anakupenda au hakupendi. Itakuwa ni hatari sana endapo utakayetokea kumpenda atakuwa hana hata chembe ya penzi kwako lakini akakukubalia kwa kukutamani tu. Hapo tarajia maumivu. Hata hivyo, hayo yote ni maisha, mwisho wa siku unatakiwa kujua kwamba, binadamu mwenzako hana nafasi ya kukukosesha furaha. Kila jambo anapanga Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, kama leo hii huyo uliyenaye anakusababisha uchanganyikiwe kiasi cha kutoona furaha ya maisha, unatakiwa kuamini kwamba hayo ni mapito na siku za furaha zinakuja kwako. Mungu siku zote hawezi kumtupa mja wake, hata kama leo hii mapenzi yanakutesa, usione kwamba Mungu kakutupa, usidhani Mungu hayaoni machozi yako. Yawezekana anakupa mtihani wa kukupima kisha aone utafanya nini au utasema nini. Wewe jiulize kwamba kwani ni lipi ambalo umemkosea mpaka awape furaha wengine wewe akufanye mtu wa kulia kila siku? Kubaliana na hali hiyo kwa sasa lakini amini siku si nyingi machozi unayotoa yatabaki historia hapo baadaye. Sisemi hivyo kwa kukutia moyo tu bali hata wewe mwenyewe utakuwa umeshuhudia watu ambao huko nyuma walikuwa kama wewe lakini leo hii ni watu na wapenzi wao, ni watu na waume/wake zao, tena katika maisha mazuri. Kwa sasa endelea kucheza kamari. Kama moyo wako umempenda mtu fulani, endelea kumpenda na kama atakuwa anakutenda, vumilia katika yale yanayovumilika. Ukiona amezidi na moyo wako unasita kuendelea kuwa naye, hata bila kuomba ushauri kwangu au kwa mtu mwingine, muweke pembeni kisha ishi maisha yako. Jamani kwa leo naomba niishie hapo nikiamini kwamba wale wanaoteswa na mapenzi, nimepandikiza mbegu mpya katika mioyo yao. Tujiepushe tu na kusema, ‘mimi sitakuja kupenda tena’ eti kwa sababu mtu uliyekuwa naye kakutenda. Huwezi kuishi peke yako milele, mwenza ni kitu muhimu katika maisha na kumbuka uliye naye sasa siye ambaye utampata kesho, watu wanatofautiana

Wednesday, January 12

Huamini nini !!!...yule demu huyu hapa....!!!!?

'''mh hichi kisiki kama unafunga nacho pingu za maisha ...jiandae kutapika nyongo kila siku....

''walimtokea wote walikuwa na bullet.....
'''yaani nikipata kamume mbuzi mbona katajuta ...ntakaminya kama nnavyominya chawa..
Anaesema mwanamke hana misuli haya hiyo hapo yote ...
kama akiamua kukuchota mtama ujue anakugawa vipande viwili....

ukimaliza kuangalia na kusoma omba dua .....!!!


Shukrani wakazi wa Arusha, nia yetu ni moja na kwa umoja wetu tutafikia malengo. Ndugu zetu wakapumzike kwa amani na damu yao iwe chachu ya kupatikana kwa ukombozi wetu

Monday, January 10

FACEBOOK WILL END ON MARCH 15th!

PALO ALTO, CA –Mark Zuckerberg announced that Facebook will be shut down in March. Managing the site has become too stressful.

“Facebook has gotten out of control,” said Zuckerberg in a press conference outside his Palo Alto office, “and the stress of managing this company has ruined my life. I need to put an end to all the madness.”

Zuckerberg went on to explain that starting March 15th, users will no longer be able to access their Facebook accounts.

“After March 15th the whole website shuts down,” said Avrat Humarthi, Vice President of Technical Affairs at Facebook. “So if you ever want to see your pictures again, I recommend you take them off the internet. You won’t be able to get them back once Facebook goes out of business.”

Zuckerberg said that the decision to shut down Facebook was difficult, but that he does not think people will be upset.

“I personally don’t think it’s a big deal,” he said in a private phone interview. “And to be honest, I think it’s for the better. Without Facebook, people will have to go outside and make real friends. That’s always a good thing.”

Some Facebook users were furious upon hearing the shocking news.

“What am I going to do without Facebook?” said Denise Bradshaw, a high school student from Indiana. “My life revolves around it. I’m on Facebook at least 10 hours a day. Now what am I going to do with all that free time?”

However, parents across the country have been experiencing a long anticipated sense of relief.

“I’m glad the Facebook nightmare is over,” said Jon Guttari, a single parent from Detroit. “Now my teenager’s face won’t be glued to a computer screen all day. Maybe I can even have a conversation with her.”

Those in the financial circuit are criticizing Zuckerberg for walking away from a multibillion dollar franchise. Facebook is currently ranked as one of the wealthiest businesses in the world, with economists estimating its value at around 7.9 billion.

But Zuckerberg remains unruffled by these accusations. He says he will stand by his decision to give Facebook the axe.

“I don’t care about the money,” said Zuckerberg. “I just want my old life back.”

The Facebook Corporation suggests that users remove all of their personal information from the website before March 15th. After that date, all photos, notes, links, and videos will be permanently erased.

Friday, January 7

comin home .....welcom Diddy

Thursday, January 6

Amitha Bachchan anakula bata kwa kwenda mbele..

''niacheni jamani nile jasho langu....movie ngapi nimewatengenezea..???'
''mh kweli filamu zinalipa next tym na mke wangu......nimewachia Abhisheki mtakoma nae....''
''natamani hichi kiboti...kipae hadi mawinguni''
Bollywood star Amitabh Bachchan rides on a jet ski at Benaulim beach in Goa.

Every one has his dream........ze comedy cornerVimeo.........produ..........


kina nini...kiuno???,....kifafanue....

Wednesday, January 5

Jamani mchumba wa Dr..Slaa.....!!!!Hivi ndivyo hali ilivyokuwa mjini Arusha jana. Viongozi wa juu wa Chadema wamekamatwa wengine wamejeruhiwa vibaya, akiwemo mchumba wa Dk. Slaa, Bi Josephine'pichani' mshike mshike uliotokea baada ya chama cha chadema kuzuiliwa kufanya maandamano yaliyoandaliwa na chama hicho

''Napendwa na wanawake mpaka nawaomba wapunguze''

breaking nyuuuuuuuu.Z.....A.TOWN KUMENUKA...JIONI HIII


Viongozi wa CHADEMA katika maandamano leo kabla
ya kutawanywa na polisi na wengine kutiwa mbaroni
Maandamano ya wanaosadikiwa kuwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA yakikatisha mitaa ya jiji la Arusha muda mfupi uliopita
Polisi wayapiga stop maandamano hayo
Maandamano yakiwa yamepigwa stop
Maeneo ya unga limited
Arusha hapatoshi dakika hii.
Picha na Aravind BK
MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI MH. FREEMAN MBOWE NI MIONGONI MWA VIONGOZI KADHAA WA CHAMA HICHO AMBAO WAKO MIKONONI MWA POLISI JIJINI ARUSHA DAKIKA HII, BAADA YA KUTIWA MBARONI KWA KILE KILICHOONEKANA KUWA MAANDAMANO BATILI.

TIMU YA GLOBU YA JAMII AMBAYO IKO ENEO LA TUKIO LIMEWATAJA VIONGOZI WENGINE WALIO KOROKORONI KUWA NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH. GODBLESS LEMA, MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI NA WANACHAMA WENGINE KADHAA WA CHADEMA.

HABARI ZINASEMA POLISI WALITAWANYA MAANDAMANO HAYO YALIPOKARIBIA OFISI ZA TAKUKURU NA KWAMBA BAADA YA VUTA NIKUVUTE, MH. MBOWE NA WENZIE WAKAKAMATWA NA KUTUPWA RUMANDE.

AIDHA HABARI ZINADATISHA KWAMBA JIJI LA ARUSHA LINARINDIMA KWA MPAMBANO WA KUKIMBIZANA WA POLISI NA MAKUNDI YA WATU WANAODAIWA KUTAKA KWENDA KITUO CHA POLISI KUWATOA WALIOKAMATWA KWA NGUVU.
--------------------------------

Mh. Freeman Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka Arusha jana jioni alisema maandamano hayo yatakayohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi ulio kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni.

Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka jijini Arusha jana jioni alisema CHADEMA itaanza rasmi kuitumia nguvu ya umma kupinga kile alichokiita "uhuni uliofanywa na CCM na serikali yake kujipa ushindi wa lazima katika uchaguzi wa umeya kinyume na matakwa ya sheria halali za nchi.

"Mwanza hakujafanyika uchaguzi kwa sababu ya dhuluma, Kigoma na Arusha uchaguzi ulikuwa batili kabisa. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) tumemsihi sana aingilie kati lakini ameendelea kushirikiana na chama chake (CCM) kuinyima CHADEMA haki ya kuongoza. Tunakwenda kulaani kwa nguvu zote uchakachuaji wa maamuzi ya wananchi" alisema Mbowe. Kwa chanzo na habari kamili....

BOFYA HAPAkikwete mikononi mwa Bi kidude....Moshi washangaaTuesday, January 4

Je.unajua ni kwanini wakina*****wanatembea na picha za wakina bontona kwenye pochi zao!!!


Wiki iliyopita tulianza somo hili lenye mada kuhusu dondoo zinazoweza kusaidia kuimarisha mapenzi, bila kupoteza muda tuendelee kutoka pale tulipoishia.

TENDO LA NDOA: Wataalamu wameandika mengi kuhusu umuhimu wa kutoshelezana kwenye tendo la ndoa, hivyo sipendi kueleza mengi lakini pengine nijazie kwa kusema kuwa mazungumzo juu ya kuridhishana na sehemu muafaka za kusisimuana ni vyema yakapewa kipaumbele ili kila upande uhudumiwe na kufurahia tendo ipasavyo.

KUAMBATANA: Tumeangalia dondoo inayoelezea umuhimu wa wapenzi kuambatana kwenye matembezi yao, lakini sehemu hii tunaelezea umuhimu wa kwenda kwenye manunuzi ya mahitaji mkiwa pamoja. Kitendo hiki hujenga mapenzi kwa kiwango cha juu na huchochea hamasa ya kila mmoja kujiona ni sehemu ya mwenzake.

KUSHIKANA: Mnapokuwa kwenye matembezi yenu ya jioni, mnashauriwa kuwa na tabia ya kushikana mikono au sehemu nyingine yoyote ya mwili. Kitendo hiki hufuta hisia za kuoneana aibu mbele za watu na huongeza uaminifu kwa wapenzi.
TENDO ALILOTAKA KUTENDA: Ikiwa mwenza wako aliwahi kukuambia kuwa anakusudia kufanya jambo fulani, unachotakiwa wewe ni kujiandaa kwa upande wako na kulifanya bila kumwambia.Kwa mfano, “Mpenzi wangu niliwahi kusikia unataka kununua kabati la vyombo, tayari lipo ndani kwetu.”

SIKILIZA: Kusikilizana ni jambo muhimu. Mpenzi wako anapokuambia kitu unatakiwa kumsikiliza, ni vibaya kuwa na maamuzi ya upande mmoja kwani utamfanya mwenzako ajisikie vibaya hasa pale anapokushauri jambo zuri lenye manufaa kwa maisha yenu halafu wewe usilitende.
KULA PAMOJA: Kitendo cha wapenzi kuamua kutoka na kwenda kwenye mgahawa kula chakula cha jioni pamoja huchochea hisia za mapenzi. Mbali na hilo, jenga penzi lako kwa kupendelea kula chakula na umpendaye.

KUTAZAMA PICHA: Inapendeza sana wapenzi wakitafuta sehemu tulivu na kutumia muda wao kutazama picha zao za utoto au zile walizopiga mwanzo wa penzi lao na kukumbushana hali ilivyokuwa wakati huo. Kusema kweli ni kitendo kilichothibitika kuchochea hamasa za mapenzi.
KUHUSU CHAI: Chai ya asubuhi ya wapendanao ni vyema ikanywewa chumbani, hasa kama wote ni wafanyakazi au mmoja wao. Usiulize kwa nini isiwe sebuleni, ni kwa sababu ya kutoa fursa ya kuhudumiana kwa ukaribu na uhuru zaidi kama wapenzi. Ila kama wapenzi hunywa chai ya kifamilia si vibaya wakiungana na jamaa zao, ila wakakaa karibu.

KUCHANGIA FARAGHA: Kuna mambo mengi yanayohusu faragha za wapenzi, hivyo ni vyema kuwa na desturi ya kushirikishana na kuyachangia kwa pamoja. Mfano kutazama video za mapenzi, kuelimishana kuhusu mitindo na mambo ya siri.
MIRADI YA PAMOJA: Mnapokuwa wapenzi mnaoaminiana ni vizuri kuwa na miradi na mipango ya kimaendeleo ya pamoja na ikiwezekana ushirika wenu uwe wazi ili kuufanya kila upande ujione ni sehemu ya mafanikio. Haifai mwanaume au mwanamke kuendesha maisha yake peke yake (kujenga nyumba, kununua kiwanja), bila kumshirikisha mwenzake.

KUKUMBUSHANA: Kichocheo kingine cha mapenzi ni kuwa na tabia ya kukumbushana mambo yenu ya zamani. “Unakumbuka ulipokuja kunitorosha siku ile usiku, halafu tukakutana na baba?” Kifupi kumbukumbu huleta hali ya mtu kujitambua alikotoka na aendako, kukumbushana huko kusiwe kwa mambo ya zamani tu bali kwa kila jambo linaloonekana kusahaulika na upande mmoja.

KUOGA PAMOJA: Wapenzi wengi hupuuza sana tendo la kwenda bafuni kuoga pamoja, wanawake wengi hudhani kuwa kumpelekea mume wake maji bafuni au kumuandalia taulo inatosha, hapana! Kwa kadiri muwezavyo pendeleeni kuoga pamoja, kwani kuoga pamoja husaidia kujenga hisia za kimapenzi.
KUBEBA PICHA YA MWENZA WAKO: Inafahamika kuwa wanaume hubeba ‘waleti’ na wanawake huwa na pochi ambazo wataalamu wanashauri ziwe na picha za wale wanaowapenda, si kwa faida yao lakini ni ya wapenzi wao ambao hutajwa kujisikia vizuri wanapotambua kuwa wamepewa kipaumbele kwa kuwekwa kwenye waleti au pochi.

Itaendelea wiki ijayo...

Naipenda mimba kuliko mtoto mwenyewe....


Sunday, January 2

Msiba wa mtanzania Hyderabad india

Marehemu shakir Hamdoun Al-marhubi
Marehemu alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Osmania UNIV,kilichoko hapa hyderabad,alikuwa anasoma kozi ya BCA (post graduate)
Marehemu alikutwa nyumbani kwake amefariki dunia lakini mpaka sasa taarifa za kifo chake hazijajulikana ,mwili wa marehemu umepelekwa Gandhi hospital kwa uchunguzi zaidi


Marehemu mwenye shati nyekundu akiwa na rafiki zake hapa hyderabad

Marehemu wa pili kutoka kulia enzi za uhai wake hapa akiwa uwanjani masab tank
wa tatu kutoka kushoto kwako ..akiwa kwenye sherehe ya mahafali ya wa wanafunzi tsah
Mkiti mstahafu TSAH Bw,Nkya akiwa mazishini sainikpuri
Mkiti wa kamati ya starehe TSAH mstahafu mwenye aliyevaa shati nyekundu alikuwepo kwenye mazishi na ndie aliyetayarisha hizi picha ...
Mwenye fulana nyeusi ktkt Mr Abdul Aziz ndie alikuwa mtu wake wa karibu sana
kwenye mazishi sainikpuri


Aliyesimama ni sheikh Mohammed Best akitoa mawaidha kwenye mazishihii ndio nyumba mazishi yalipofanyikia
kwa kweli wanafunzi walishikwa na simanzi sana


walijitokeza wanafunzi wengi sana ,kuonesha kuwa bado wanampenda ndugu yao
TULIKUPENDA SANA NDUGU YETU LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI
tunamuomba Mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi
AMIN